-
Mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa yaliongezeka sana mwaka 2025
Jan 10, 2026 03:12Duru za Palestina zimeripoti kwamba mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuvunjia heshima eneo hilo takatifu yaliongezeka kwa kiwango kikubwa katika mwaka uliomalizika majuzi wa 2025 na kwamba mashambulizi hayo yaliandamana na ujumbe wa kisiasa na kidini.
-
Hamas yatahadharisha, Israel itasambaratisha makubaliano ya kusimamisha vita
Jan 10, 2026 02:08Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa ikizungumzia ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel na kutahadharisha kuwa makubaliano hayo yako kwenye ukingo wa kusambaratika.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi uendeshaji wa Ghaza kwa kamati ya shakhsia wa kujitegemea
Jan 09, 2026 23:04Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, harakati hiyo ilishaamua tokea huko nyuma kwamba haitakuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika hatua yoyote ya upangaji wa masuala ya kiidara na kiuendeshaji ya siku za usoni katika Ukanda wa Ghaza.
-
UNRWA: Misaada inayoingia Gaza inakabiliwa na vivingiti shadidi vya Israel
Jan 09, 2026 07:30Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Wapalestina (UNRWA) limetangaza kuwa vizingiti vilivyowekwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika njia za kuingia Ukanda wa Gaza vimesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa misaada kwa Wapalestina katika eneo hilo.
-
Wizara ya Afya ya Palestina: Waliouawa shahidi Gaza ni zaidi ya 71,300
Jan 09, 2026 02:53Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023.
-
Utafiti: Takriban asilimia 90 ya watu katika nchi za Kiarabu wanapinga kuanzishwa uhusiano na Israel
Jan 08, 2026 22:52Idadi kubwa ya watu katika Ulimwengu wa Kiarabu wanapinga kuitambua Israel na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu. Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni wa kikanda.
-
UN yaitaka Israel ikomeshe 'mfumo wa ubaguzi wa apathaidi' inaoendesha Ukingo wa Magharibi
Jan 07, 2026 23:35Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu umesema, hatua za miongo kadhaa za Israel za kuwatenga na kuwabagua Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi inaoukalia kwa mabavu zinazidi kuongezeka, na kwa sababu hiyo umetoa wito wa kuutaka utawala huo ukomeshe "mfumo wake wa ubaguzi wa rangi wa apathaidi".
-
UAE yatuhumiwa tena na Saudia; mara hii ni kuwaunga mkono Wadruze ili kuigawanya Syria
Jan 07, 2026 23:33Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa, Saudi Arabia imetoa tuhuma zisizo za kawaida dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu, Imarati huku kukiwa tayari kuna mvutano unaoongezeka kati ya mataifa hayo mawili ya Ghuba ya Uajemi, tuhuma ambazo zinahusu wasiwasi kuhusu namna UAE inavyojihusisha na masuala ya Syria.
-
Imarati inapanga kuijengea Israel kambi ya jeshi karibu na Saudi Arabia
Jan 07, 2026 06:43Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimefichua mpango wa Umoja wa Falme za Kiarabu wa kujenga kambi ya kijeshi ya Israel karibu na mpaka wa nchi hizi mbili za Kiarabu.
-
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: Netanyahu ni mtenda jinai anayechukiwa zaidi katika historia
Jan 07, 2026 04:07Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amemtaja Waziri Mkuu wa Israel kuwa mtenda jinai anayechukiwa zaidi katika historia na kusema: "Uongo wa Benjamin Netanyahu dhidi ya miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayoendeshwa kwa malengo ya amani ulikuwa kisingizio tu cha kuhalalisha mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran.