Hamas yatahadharisha, Israel itasambaratisha makubaliano ya kusimamisha vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135312-hamas_yatahadharisha_israel_itasambaratisha_makubaliano_ya_kusimamisha_vita
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa ikizungumzia ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel na kutahadharisha kuwa makubaliano hayo yako kwenye ukingo wa kusambaratika.
(last modified 2026-02-09T08:50:53+00:00 )
Jan 10, 2026 05:38 UTC
  • Hamas yatahadharisha, Israel itasambaratisha makubaliano ya kusimamisha vita

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa ikizungumzia ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel na kutahadharisha kuwa makubaliano hayo yako kwenye ukingo wa kusambaratika.

Taarifa ya Hamas imesema mauaji ya kigaidi yanayofanywa na Israel kwa visingizio visivyo na maana yanatishia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Ukanda wa Gaza iliripoti jana Ijumaa kwamba utawala haramu wa Israel umekiuka makubaliano hayo mara 193.

Taarifa hiyo imesema, katika kipindi cha siku 90 zilizopita baada ya kuanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita malori elfu 23 na 19 tu ya misaada ya kibinadamu yameruhusiwa kuingia Gaza, wakati malori elfu 54 yalipaswa kuingiza misaada katika eneo hilo la Palestina.

Idara ya Habari ya Gaza imesema, makumi ya Wapalestina wamekufa shahidi na wengine kujeruhiwa kutokana na kuporomoka nyumba zaidi ya 50 zilizopigwa mabomu na Israel.

Idara hiyo imetahadahrisha kuhusiana na hali mbaya isiyo na kifani ya wakimbizi wanaoishi kwenye mahema yasiyo salama na uhaba wa misaada ya kibinadamu kutokana na kufungwa vivuko vya kuingia eneo hilo la Palestina.