Jihad Islami ya Palestina: Muqawama hauwezi kutokomezwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135432-jihad_islami_ya_palestina_muqawama_hauwezi_kutokomezwa
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina amesisitiza katika taarifa yake kwamba Muqawama na mapambano ya ukombozi wa Palestina ni sehemu muhimu ya taifa la Palestina na hayawezi kutokomezwa au kuangamizwa.
(last modified 2026-01-13T06:41:41+00:00 )
Jan 13, 2026 06:41 UTC
  • Muhammad Al-Hindi
    Muhammad Al-Hindi

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina amesisitiza katika taarifa yake kwamba Muqawama na mapambano ya ukombozi wa Palestina ni sehemu muhimu ya taifa la Palestina na hayawezi kutokomezwa au kuangamizwa.

Muhammad Al-Hindi amesema: "Wavamizi wanazuia mchakato wa kuunda kamati ya kiteknokrati kwa ajili ya utawala wa Ukanda wa Gaza na wanafuatilia majina yaliyochaguliwa kushiriki katika kamati hiyo."

Ameongeza kuwa: "Utawala wa Kizayuni wa Israel pia unapinga ushiriki wa mamlaka ya Ndani ya Palestina katika kusimamia Ukanda wa Gaza na unazuia hata kuwekwa bendera ya Palestina kwenye kivuko cha Rafah."

Awali, Mohammed Nazzal, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa harakati ya Hamas, alikuwa amesisitiza haja ya kuingia katika awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kuunda serikali ya kitaifa ya Palestina, na kutangaza kwamba harakati hiyo imewasilisha orodha ya awali ya majina yaliyopendekezwa kwa ajili ya kusimamia serikali hiyo.

Nazzal ametangaza kuwa makundi ya mapambano ya ukombozi wa Palestina yako tayari kumpokea Nickolay Mladenov, mratibu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Mashariki ya Kati, kama mwenyekiti wa Baraza la Amani la Gaza, badala ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair.