Shirika la UNICEF: Watoto wa Gaza wamesahauliwa na jamii na kimataifa
-
Shirika la UNICEF: Watoto wa Gaza wamesahauliwa na jamii na kimataifa
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, jamii ya imewasahau watoto wa Gaza ambao wanataabika na kuteteseka kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu na ukatili wa kutisha.
Taarifa ya UINCEF imesema, ukiukaji wa usitishaji mapigano wa utawala wa Israel huko Gaza umesababisha vifo vya watoto zaidi ya 100; kama ambavyo shirika hilo limeonya kuhusu hali mbaya zaidi ya kibinadamu huko Gaza.
Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina amesema: "Hali ya maisha ya watoto katika Ukanda wa Gaza ni mbaya kutokana na hali ya hewa ya baridi, mvua kubwa na mafuriko."
UNICEF imekosoa utendaji wa jamii ya kimataifa katika Ukanda wa Gaza na kuongeza: "dunia imeshindwa na tumewaangusha watoto wa Gaza ambao wanaendelea kufa kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika wakati wa majira ya baridi." Takwimu zinaonyesha kuwa, watoto 82 wamefariki katika Ukanda wa Gaza tangu usitishaji vita uanze kutekelezwa, jambo ambalo linashangaza na lazima likomeshwe.
Hayo yanajiri katika halia mabyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi Wapalestina (UNRWA) limetangaza kuwa vizingiti vilivyowekwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika njia za kuingia Ukanda wa Gaza vimesababisha kupungua kwa kiwango kikubwa misaada kwa Wapalestina katika eneo hilo.
Ofisi ya Habari ya Ukanda wa Gaza imesema kuwa, uchokozi unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel wa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano hadi sasa umepelekea kuuawa shahidi Wapalestina wasiopungua 425, huku wengine 1,206 wakijeruhiwa.