Qatar: Tunawasiliana ili kutatua tofauti kati ya Marekani na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135460-qatar_tunawasiliana_ili_kutatua_tofauti_kati_ya_marekani_na_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ametangaza kuwa, Doha inafanya mawasiliano na pande mbalimbali ili kutuliza hali katika eneo hili na kutatua tofauti kati ya Iran na Marekani.
(last modified 2026-02-15T09:07:51+00:00 )
Jan 14, 2026 02:42 UTC
  • Majid Al-Ansari
    Majid Al-Ansari

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar ametangaza kuwa, Doha inafanya mawasiliano na pande mbalimbali ili kutuliza hali katika eneo hili na kutatua tofauti kati ya Iran na Marekani.

"Majid Al-Ansari," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, alitangaza: "Sisi ni miongoni mwa pande zinazowasiliana na pande zingine ili kutuliza hali katika eneo hili na kutatua tofauti kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani."

Aliongeza: "Diplomasia ni njia bora na yenye ufanisi ya kutatua tofauti zilizopo katika eneo."

Al-Ansari aliendelea: "Tunashirikiana na washirika wetu na majirani zetu kwa kuzingatia njia hii ya kidiplomasia."

Matamshi haya yanatolewa wakati ambapo eneo la Asia Magharibi linakabiliwa na hali ngumu kutokana na uingiliaji kati wa Marekani na vitisho dhidi ya mataifa ya eneo, hasa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza mara kwa mara kwamba haitaacha jaribio lolote la kuvuruga usalama wa nchi bila jibu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ameionya Marekani kwamba, Tehran "iko tayari kwa machaguo yote" baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuchukua hatua za kijeshi sambamba na Iran kukabiliwa na machafuko hivi karibuni yaliyochochewa na kuungwa mkono na maadui wa nje ya nchi.

"Tuko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo ya nyuklia, mradi tu ni bila ya kutolewa vitisho au amri," ameeleza bayana Araghchi, huku akihoji kama Washington iko "tayari kweli kwa mazungumzo ya usawa na ya haki" na akasisitiza kwa kusema: "itapokuwa tayari, tutazingatia jambo hilo kwa uzito".