-
Hamas yamwambia Netanyahu: Mateka wenu ni wengi zaidi kuliko unavyofikiri; Wazayuni 300 waangamizwa katika Kimbunga cha Al Aqsa
Oct 07, 2023 23:57Abu Ubaida, msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kuwa idadi ya maafisa na wanajeshi wa Israel waliokamatwa mateka na harakati hiyo katika Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa ni kubwa zaidi kuliko anavyoamini Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na kwamba mateka hao wapo katika maeneo yote ya Ukanda wa Gaza.
-
Viongozi wa Muqawama wasujudu "Sijdatu-Shukri" kwa mafanikio ya "Kimbunga cha Al-Aqsa"
Oct 07, 2023 23:57Viongozi wa Muqawama wa Palestina wamesujudu sijda ya shukurani kwa Allah SWT baada ya vikosi vya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS kufanya kwa mafanikio mashambulio ya maroketi yaliyolenga vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza.
-
Wapalestina wateka kituo cha kijeshi, waangamiza na kuteka askari wengi wa Israel katika Operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa"
Oct 07, 2023 11:57Wapalestina leo wametekeleza operesheni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi dhidi ya Israel, ya mashambulio ya kushtukiza ambayo yamefanywa na wanamapambano waliovuka uzio na kuingia katika miji inayokaliwa kwa mabavu, sambamba na msururu mkubwa wa maroketi yaliyovurumishwa kutokea Ukanda wa Gaza.
-
Haniya: Kimbunga cha Al-Aqsa kimeanzia Gaza na kitafika hadi Ufukwe wa Magharibi
Oct 07, 2023 11:44Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: Kimbunga cha Al-Aqsa kimeanzia Gaza na kitafika hadi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, nje yake na popote pale walipo wananchi wa Palestina.
-
Jinai ya Homs; Kuongeza uwezekano wa kufufuliwa ugaidi unaoungwa mkono na Marekani nchini Syria
Oct 07, 2023 04:44Shambulio la kigaidi la Alkhamisi, Oktoba 5, kwenye sherehe ya kuhitimu mafunzo ya wanafunzi wa chuo kikuu cha maafisa wa jeshi katika mkoa wa Homs, kaskazini magharibi mwa Syria, lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 80 na kujeruhi wengine zaidi ya 240.
-
Umoja wa Mataifa walaani shambulio la utawala wa Kizayuni kusini mwa Nablus
Oct 07, 2023 04:26Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la karibuni la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakazi wa Kipalestina kusini mwa mji wa Nablus.
-
Ujumbe wa gwaride kubwa la Brigedi ya al-Quds katika kumbukumbu ya miaka 36 ya kuasisiwa Jihad Islami
Oct 06, 2023 22:55Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina lilifanya gwaride lake kubwa zaidi la kijeshi katika Ukanda wa Gaza juzi tarehe 4 Oktoba kwa mnasaba wa mwaka wa 36 wa kuasisiwa harakati hiyo.
-
Syria: Damu ya Mashahidi itaongeza azma yetu ya kupata ushindi kamili
Oct 06, 2023 07:40Ofisi ya Rais wa Syria imetoa taarifa ikizungumzia kushindwa ugaidi mbele ya irada na uwezo wa nchi hiyo na kusisitiza kwamba damu ya Mashahidi wa chuo cha kijeshi cha Homs inaongeza azma ya Damascus ya kufikia ushindi kamili.
-
Ansarullah yatangaza kushikamana na taifa la Syria
Oct 06, 2023 03:40Ofisi ya kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen imelaani mashambulizi ya makundi ya kigaidi katika chuo cha kijeshi cha Homs nchini Syria.
-
Askari makatili wa Israel wawaua shahidi vijana 2 wa Kipalestina Tulkarm
Oct 05, 2023 23:17Wanajeshi vamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi vijana wawili wa Kipalestina katika mji Tulkarm, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.