-
Rais Assad wa Syria kuelekea Saudia kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
May 18, 2023 07:56Rais Bashar al-Assad wa Syria leo anaelekea Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika jiji la Jeddah siku ya Ijumaa.
-
Mawaziri wa utawala wa Kizayuni watoa wito wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa
May 17, 2023 21:38Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa baadhi ya mawaziri na wajumbe wa bunge la utawala haramu wa Israel, Knesset, wametoa wito wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya maandamano ya bendera.
-
Bunge la Kiarabu: Kumbukumbu ya Siku ya Nakba katika Umoja wa Mataifa ni ushindi kwa Palestina
May 17, 2023 07:37Katika taarifa yake iliyotolewa kwa mnasaba wa kutimia miaka 75 ya kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina, Bunge la Kiarabu limetangaza kuwa kufanyika shughuli ya Siku ya Nakba katika Umoja wa Mataifa ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza katika taasisi hiyo ya kiimataifa, ni ushindi kwa taifa la Palestina.
-
Nakba ya Palestina iliyogeuzwa kuwa Nakba ya Israel!
May 17, 2023 04:30Licha ya mashinikizo na kampeni kubwa iliyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na Marekani ya kuzishawishi nchi mbalimbali, wanachama wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu waliadhimisha kwa mara ya kwanza kumbukumbu ya mwaka wa 75 wa maangamizi ya kizazi cha wananchi madhulumu wa Palestina katika tukio la Siku ya Nakba.
-
Kongamano la kimataifa la Palestina lafanyika Rome Italia
May 17, 2023 02:57Kongamano la kimataifa la Palestina katika sheria za kimataifa limefanyika katika ubalozi wa Palestina mjini Rome mji mkuu wa Italia.
-
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wavamia tena Masjidul-Aqswa
May 16, 2023 23:12Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali wameuvamia tena msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu.
-
Wazayuni wakiri kupata pigo; wasema: Israel haina uwezo wa kukabiliana na makombora ya Wapalestina
May 16, 2023 10:49Majenerali wa jeshi la utawala wa Kizayuni wamekiri kupata pigo katika vita vya siku tano vilivyoisha Ijumaa iliyopita na kutangaza wazi kwamba, katika uvamizi wake wa hivi karibuni huko Ghaza, utawala wa Israel si tu haukupata mafanikio yoyote, lakini ngome ya ulinzi wa anga ya Israel imeshindwa kukabiliana na makombora ya muqawama wa Palestina.
-
Arab League: Kushiriki Syria katika mkutano wa Jeddah ni mwanzo wa awamu mpya
May 16, 2023 10:47Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, kikao cha awali cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii kilichofanyika mjini Jeddah kimejadili masuala muhimu ya kijamii kwa ajili ya ushirikiano wa nchi za Kiarabu.
-
Rais wa Palestina autaka Umoja wa Mataifa usimamishe uwanachama wa Israel
May 16, 2023 03:11Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameuhimiza Umoja wa Mataifa usimamishe uwanachama wa utawala haramu wa Israel katika chombo hicho kikuu cha dunia mpaka utakapokomesha uchokozi na ukandamizaji wake dhidi ya Wapalestina na kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa ya uundaji mataifa mawili tofauti ya Israel na Palestina na kutekelezwa haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea makwao.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria awasili Saudia kushiriki mkutano wa mawaziri wa Arab League
May 16, 2023 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ameelekea Saudi Arabia akiongoza ujumbe wa nchi yake kushiriki vikao vya utangulizi vya Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.