-
Hizbullah ya Lebanon yawapelekea misaada waathirika mitetemeko ya ardhi nchini Syria
Feb 13, 2023 03:59Msafara wa misaada wa Lebanon chini ya jina la "Kampeni ya Huruma" kwa watu waliokhasiriwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria unaelekea kwenye maeneo hayo hivi sasa.
-
HAMAS: Njama za Marekani za kuisambaratisha Intifadha zitafeli
Feb 12, 2023 23:05Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu HAMAS amesema njama za Marekani za kutaka kuisambaratisha Intifadha ya Tatu ya Wapalestina dhidi utawala wa Kizayuni wa Israel zitagonga mwamba.
-
Hizbullah yalaani hatua ya Marekani ya kuzuia misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa wa zilzala nchini Syria
Feb 12, 2023 08:22Afisa wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amekosoa vikali hatua ya kimaonyesho ya Marekani eti ya kutenga msaada kwa ajili ya waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Syria na Uturuki na kutangaza kuwa kiasi cha fedha za msaada huo uliotangazwa na Washington baada ya kukosolewa sana kwa kuzuia misaada kwa waathiriwsa wa tetemeko la ardhi ni sawa na siku moja ya wizi wa mafuta unaofanywa na Marekani kwenye visima vya mafuta vya kaskazini mwa Syria.
-
Tahadhari kuhusu ukosefu wa dawa nchini Yemen, kifo kinawanyemelea wagonjwa wa figo
Feb 12, 2023 08:14Afisa wa Wizara ya Afya ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameonya kuwa zaidi ya wagonjwa elfu tano wa figo wako katika hatihati ya kufariki dunia kutokana na ukosefu wa dawa.
-
Assad akosoa undumakuwili wa Magharibi kuhusu hali ya kibinadamu katika Syria iliyokumbwa na zilzala
Feb 12, 2023 03:45Rais wa Syria Bashar al-Assad amekosoa misimamo ya kundumakuwili ya nchi za Magharibi katika kukabiliana na wahanga wa mitetemeko mikubwa ya ardhi iliyokumba Syria na Uturuki, akisema mataifa ya Magharibi hayajali hali ya kibinadamu nchini kwake.
-
Zilzala Uturuki na Syria: Waliofariki wakaribia 30,000, UN yaonya idadi ni mara mbili ya hiyo
Feb 12, 2023 01:07Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 6 baada ya maafa hayo ambapo idadi ya walipoteza maisha inakaribia 30,000 huku Umoja wa Mataifa ukitabiri kuwa yamkini idadi hiyo ikaongezeka maradufu.
-
POLITICO: Saudia kutumia mabilioni ili iwe mwenyeji wa Kombe la Dunia
Feb 11, 2023 23:06Saudi Arabia imeripotiwa kutoa pendekezo kwa siri la kuwa tayari kugharamia ujenzi wa miundombinu yote kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotazamiwa kufanyika Ugiriki na Misri mwaka 2030.
-
Syria yakosoa 'upotoshaji' wa Marekani kuhusu kuondoa vikwazo
Feb 11, 2023 23:05Serikali ya Syria imekosoa vikali hatua ya Marekani ya kutangaza kuisimamishia vikwazo nchi hiyo ya Kiarabu kwa muda wa miezi sita, eti ili kuruhusu kupelekwa misaada ya dharura katika taifa hilo lililokumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi hivi karibuni.
-
Baada ya kupita siku 5, manusura wa tetemeko la ardhi waendelea kupatikana vifusini nchini Uturuki
Feb 11, 2023 08:27Watu kadhaa wameokolewa leo nchini Uturuki kwa kutolewa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, wakati vikosi vya uokoaji kutoka nchi mbalimbali duniani vikiongeza kasi ili kujaribu kuokoa maisha ya watu zaidi baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumatatu kusini mwa nchi hiyo na katika nchi jirani ya Syria.
-
Idadi ya waliofariki dunia yapindukia 24,000 zilzala ya Syria na Uturuki, matumaini ya kupata manusura zaidi yanafifia
Feb 11, 2023 03:56Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa na zizlala ya Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 5 baada ya maafa ya tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 24,000 na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine.