Hizbullah ya Lebanon yawapelekea misaada waathirika mitetemeko ya ardhi nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i93994-hizbullah_ya_lebanon_yawapelekea_misaada_waathirika_mitetemeko_ya_ardhi_nchini_syria
Msafara wa misaada wa Lebanon chini ya jina la "Kampeni ya Huruma" kwa watu waliokhasiriwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria unaelekea kwenye maeneo hayo hivi sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 13, 2023 03:59 UTC
  • Hizbullah ya Lebanon yawapelekea misaada waathirika mitetemeko ya ardhi nchini Syria

Msafara wa misaada wa Lebanon chini ya jina la "Kampeni ya Huruma" kwa watu waliokhasiriwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria unaelekea kwenye maeneo hayo hivi sasa.

Adnan al-Muqaddam, mkurugenzi wa masuala ya usalama na huduma kwa raia wa Hezbollah ya Lebanon, amemwambia mwandishi wa televisheni ya Al Alam kwamba, msafara wa kwanza wa misaada ya Lebanon umeanza safari yake kuelekea Syria kutoka meidani ya Ashura al Hadath ukijumuisha malori 23. Malori 20 kati yake yanatokea Beirut na malori matatu yataungana na msafara huu katika eneo la Beqaa.

Ameongeza kuwa msafara huo utaelekea katika mji wa ladhiqiyyah (Latakia) na utakabidhiwa kwa shirika la Hilali Nyekundu ya Syria na gavana wa mji huo.

Al Muqaddam amefafanua zaidi kwa kusema: Msafara huo una chakula, madawa na vifaa vya afya na baadhi ya mahitaji muhimu kwa ajili ya waathiriwa wa mitetemeko mikubwa ya ardhi nchini Syria.

Afisa huyu wa Hizbullah ya Lebanon pia amesema, misafara mingine inatayarishwa na makundi ya kiraia, taasisi na wakazi wenye mafungamano na Hizbullah katika ngazi mbalimbali za afya na kijamii kwa ajili ya wahanga wa mitetemeko ya ardhi ya Syria.