-
Yemen: Zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya muungano wa Saudia
Nov 23, 2022 04:33Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imetangaza kuwa zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa Saudi Arabia.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vikali hukumu za kukatwa watu vichwa Saudi Arabia
Nov 22, 2022 23:09Mmoja wa wasemaji wanaohusika na haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea masikitiko yake kuhusu utekelezwaji wa hukumu za vifo kwa kukata watu vichwa nchini Saudi Arabia.
-
Shtayyeh: Serikali mpya ya Israel inajiandaa kutangaza vita dhidi ya Wapalestina
Nov 22, 2022 08:01Waziri Mkuu wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema, serikali mpya ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel chini ya uongozi wa wanasiasa wa mrengo wa kulia wenye misimamo ya kufurutu ada inajiandaa kutangaza vita dhidi ya Wapalestina.
-
Bunge la Waarabu lalaani hatua ya Uturuki ya kuwakatia maji raia milioni moja wa Syria
Nov 22, 2022 07:55Muungano wa Mabunge ya Nchi za Kiarabu umelaani hatua ya Uturuki ya kuwakatia maji raia zaidi ya milioni moja wa Syria katika mkoa wa al-Hasakah.
-
Kuongezeka watoto wa Kipalestina katika magereza ya Israel
Nov 22, 2022 07:09Wizara ya Mateka na Wafungwa wa Kipalestina Walioachiliwa Huru kutoka gerezani imetangaza kuwa, hivi sasa kuna watoto 170 wa Kipalestina katika magereza ya Israel huku watano kati yao wakishikiliwa pasi na kuelezwa tuhuma na makosa yao.
-
Yemen yazima jaribio la meli ajinabi kuiba mafuta yake
Nov 22, 2022 03:47Vikosi vya jeshi la Yemen vimetangaza habari ya kufanikiwa kuzima jaribio la wizi wa mafuta ya nchi hiyo, lililofanywa na meli ya kubeba mafuta ya nchi ya kigeni.
-
Bin Salman na Bin Zayed hawana ubavu isipokuwa wa kuua watoto wa Kiyemen
Nov 21, 2022 22:53Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo faili la jinai za kivita la Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Sheikh Muhammad bin Zayed Al-Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko nchini Yemen linavyozidi kuwa kubwa.
-
Kombe la Dunia; Vijana wa Kiarabu wakataa kuzungumza na wanahabari wa Israel
Nov 21, 2022 07:55Mashabiki wa soka wa nchi za Kiarabu wamekataa kuzungumza na waandishi wa habari wa mashirika ya utawala haramu wa Israel nchini Qatar, kunakofanyika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu 2022; kuonyesha upinzani wao wa kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala huo bandia unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
-
Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Nov 21, 2022 07:23Sambamba na kuanza uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita nchini Afghanistan unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito wa kuchunguzwa mashambulio ya mauaji ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
-
Idadi ya watoto waliouawa vitani nchini Yemen yapindukia 8,000
Nov 21, 2022 03:06Taasisi moja ya masuala ya sheria imetangaza kuwa, idadi ya watoto waliofanywa wahanga wa vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen imeshapindukia elfu 8.