-
UN:Israel imebomoa Majengo 44 ya Wapalestina katika kipindi cha wiki mbili
Sep 19, 2022 06:41Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa utawala ghasibu wa Israel umebomoa majengo 44 ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ikiwa ni muendelezo wa siasa zake za unyakuzi wa ardhi za Palestina kinyume cha sheria.
-
Sisitizo la Nasrullah juu ya ulazima wa kuendelezwa Muqawama wa kukabiliana na adui Mzayuni
Sep 19, 2022 04:53Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, Muqawama ndio njia pekee ya kukabiliana na adui mzayuni. Nasrullah ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa siku ya Jumamosi kwa mnasaba wa Arubaini ya Imam Hussein AS.
-
Wafanyaziara milioni 1 na nusu watembelea Samarra Iraq baada ya Arubaini
Sep 19, 2022 02:44Mji wa Samarra wenye haram mbili tukufu za Maimam wa Ahlul Bayt wa Bwana Mtume Muhammad SAW umeshuhudia wimbi kubwa la wafanyaziara waliolekea mjini humo baada ya kushiriki kwenye Arubaini ya Imam Husain AS huko Najaf na Karbala nchini Iraq.
-
Kuhuishwa uhusiano wa Hamas na Syria; kuimarisha muqawama katika eneo
Sep 18, 2022 06:47Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa inataka kuwa na uhusiano imara na Syria katika fremu ya uamuzi wake wa kuanzisha tena uhusiano na serikali ya Damascus.
-
Wafanyaziara milioni 24 washiriki matembezi Arbaeen ya Imam Hussein AS huko Karbala, Iraq
Sep 17, 2022 23:10Wafanyaziara milioni 24 wamekusanyika katika mji wa Karbala wa Iraq kuadhimisha Arbaeen, tukio la kila mwaka ambalo linaadhimisha siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa madhehebu ya Shia.
-
Nasrullah: Macho na makombora yetu yameelekezwa kwenye medani ya gesi ya Karish
Sep 17, 2022 07:29Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema leo Jumamosi kwamba macho na makombora ya harakati hiyo yameelekezwa kwenye medani ya gesi ya Karish, ambao inazozaniwa baina ya Lebanon na utawala haramu wa Israel.
-
Umoja wa Mataifa waeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya Ukingo wa Magharibi
Sep 17, 2022 07:26Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Amani Mashariki ya Kati amelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwsa mabavu.
-
Miaka arubaini baada ya jinai ya Israel ya Sabra na Shatila
Sep 17, 2022 06:29Septemba 16, inasadifiana na kumbukumbu ya miaka 40 ya jinai iliyotekelezwa na utawala haramu wa Israel huko Sabra na Shatila nchini Lebanon .
-
Askofu wa Othodoksi Palestina: Kupita kwa muda hakutafanya jinai za maghasibu wa Baitul Muqaddas zisahaulike
Sep 17, 2022 03:00Askofu Mkuu wa Kanisa la Othodoksi mjini Baitul Muqaddas (Jerusalem) amesema: Palestina haitafunga mikono na kusimama kizembe katika kukabiliana na upendeleaji unaofanywa na Magharibi kwa utawala ghasibu wa Kizayuni pamoja na sera na jinai zake.
-
Mwanachuoni Msuni wa Iraq: Tunaona fakhari kuwa wenyeji wa mazuwari wa Imam Husain
Sep 16, 2022 20:55Mkuu wa Jumuiya ya Ahlu Sunna Waljamaa ya Iraq amesema kuwa, hivi sasa Waislamu wa Iraq wanaonesha kivitendo mfano bora kabisa wa ukarimu kwa kuwahudumia kwa moyo mmoja wafanyaziara wa Imam Husain AS kutoka kila kona ya dunia.