-
HAMAS: Watawala Waarabu waliohadaiwa waangalie upya uamuzi wao
Jul 09, 2022 22:15Mkuu wa ofisi ya uhusiano na nchi za Kiarabu na Kiislamu ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, watawala Waarabu waliohadaiwa wakaanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, waangalie upya uamuzi wao huo waliochukua.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Saudia inawazuia baadhi ya Waislamu kutekeleza Hija kwa sababu za kisiasa
Jul 09, 2022 05:18Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, utawala wa Saudi Arabia unawazuia baadhi ya Waislamu kutekeleza ibada ya Hija kwa sababu ya misimamo ya kisiasa ya ukoo wa Aal Saud au misimamo ya Marekani na Israel dhidi ya Waislamu hao.
-
Makundi ya muqawama Palestina yamkosoa Abbas kukutana na Gantz
Jul 09, 2022 03:05Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amekosolewa vikali na makundi ya muqawama ya Palestina, kwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benny Gantz.
-
EU yaonya kuhusu Israel kuwatimua Wapalestina Masafer Yatta
Jul 08, 2022 23:04TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia mwandamizi wa Umoja wa Ulaya ameelezea wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa idadi kubwa ya Wapalestina kuhamishwa kwa nguvu kutoka eneo la mashambani katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kukosolewa safari ya Joe Biden Saudi Arabia na katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu
Jul 08, 2022 21:47Mbali na kuwa safari ya Rais Joe Biden wa Marekani huko Saudi Arabia na vilevile katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel imekosolewa sana lakini kile kinachodhihirika zaidi katika ukosoaji huo ni kuwa kufanyika safari hiyo sambaba na siku za kutekelezwa ibada tukufu ya Hija ni jambo ambalo haliwezi kuwa limefanyika hivi hivi bali limepangwa kufikia malengo maalumu.
-
Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Allah wasimama Arafa
Jul 08, 2022 06:01Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu wanasimama katika uwanja wa Arafa hii leo Ijumaa, kisimamo hicho kikiashiria kilele cha ibada tukufu ya Hijja.
-
Brigedi ya Al-Quds: Walowezi wa Kizayuni hawana budi ila kuondoka Palestina
Jul 08, 2022 03:41Kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 8 wa Vita vya ‘al-Buniyan al-Marsus’, Brigedi ya Quds tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami huko Palestina imetangaza kuwa itaendeleza njia ya muqawama na mapambano dhidi ya Wazayuni maghasibu na kusisitiza kuwa: Walowezi wa Kizayuni hawana budi ila kuondoka katika ardhi yote ya Palestina.
-
Mkutano wa kihistoria kati ya Haniyah na Abbas baada ya miaka 15
Jul 07, 2022 22:01Ismail Haniyah, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Mahmoud Abbas, mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, wamekutana baada ya miaka mingi ya uhusiano wa pande mbili kukatika.
-
Ibada ya Hija yaanza katika Mji Mtakatifu wa Makka
Jul 07, 2022 07:58Ibada ya kila mwaka ya Hija imeanza rasmi leo Alhamisi katika mji mtakatifu wa Makka, ikiashiria hatua kubwa kuelekea hali ya kawaida baada ya miaka miwili ya janga la corona ambapo idadi ya Mahujaji ilipunguzwa sana.
-
Rais wa Lebanon: Karibu tutafikia mwafaka na Israel juu ya uainishaji mipaka ya baharini
Jul 07, 2022 06:54Rais Michel Aoun wa Lebanon ametangaza kuwa, karibuni hivi suala la uanishaji mipaka ya baharini baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel litapatiwa ufumbuzi na kwamba njia hiyo ya utatuzi wa mzozo huo itaridhiwa na pande zote.