-
Ansarullah: Mapambano yataendelea hadi kila shibri ya ardhi ya Yemen itakapokombolewa
Oct 28, 2021 03:54Msemaji wa kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansarullah amesisitiza kuwa, mapambano dhidi ya wavamizi wa Yemen wanaoongozwa na Saudia yataendelea mpaka itakapokombolewa kila shibri ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Kundi la kigaidi la DAESH laua raia wengine kadhaa wasio na ulinzi wa Iraq mkoani Diyala
Oct 27, 2021 09:31Duru za usalama za Iraq zimetangaza kuwa, magaidi wa kundi la ukufurishaji la DAESH (ISIS) wameshambulio kijiji kimoja mkoani Diala na kuwaua na kuwajeruhi raia kadhaa wasio na ulinzi.
-
Makundi ya muqawama yaonya kuhusu kuendelea hujuma dhidi ya maeneo matakatifu Palestina
Oct 27, 2021 04:39Makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina yameuonya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na kuendelea uvamizi na hujuma dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiiislamu huko Palestina hususan makaburi ya al-Yusufiya huko Quds inayokaliwa kwa mabavu.
-
Hassan bin Abdullah al Ghanim achaguliwa kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Qatar
Oct 27, 2021 00:36Hassan bin Abdullah al Ghanim amechaguliwa kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Qatar baada ya kupigiwa kura 37 za 'ndiyo' na wabunge wa bunge hilo lililoundwa kupitia uchaguzi wa hivi karibuni.
-
Kuendelea kupuuza Israel upinzani wa walimwengu kwa ujenzi wa vitongoji vya walowez wa Kizayuni
Oct 27, 2021 00:35Uamuzi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wa kujenga nyumba nyingine mpya katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan umekabiliwa na upinzani mkali wa Umoja wa Ulaya na baadhi ya mataifa katika eneo la Asia Magharibi.
-
Umoja wa Mataifa wataka kufunguliwa vivuko vya Ghaza huko Palestina
Oct 26, 2021 08:47Umoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uheshimu sheria za kimataifa na uache kuuzingira Ukanda wa Ghaza. Umoja huo umeitaka Israel ifungue vivuko vyote vya kuingia na kutoka katika ukanda huo.
-
Jeshi la Iraq laendelea kushirikiana na al Hashd al Shaabi kupambana na magaidi
Oct 26, 2021 08:45Vikosi mbalimbali vya jeshi la Iraq vinaendelea kushirikiana na harakati ya kujitolea ya wananchi wa nchi hiyo maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi kupambana na magaidi kusini mwa mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq.
-
Jasusi wa zamani wa Saudia: Bin Salman ni katili, ana matatizo ya kiakili
Oct 26, 2021 04:36Afisa wa zamani wa Idara ya Ujasusi wa Saudi Arabia amemtaja Mohammad bin Salman, mrithi wa ufalme wa Saudia kama mtu katili, asiye na chembe ya utu na mwenye matatizo ya kisaikolojia.
-
Wasyria waandamana kushinikizi kuondoka vikosi vamizi vya Uturuki
Oct 26, 2021 04:33Mamia ya wananchi wa Syria wamefanya maandamano katika mkoa wa Aleppo (Halab), kaskazini magharibi mwa nchi kulaani uwepo wa wanajeshi vamizi wa Uturuki katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Wanawake 33 wa Kipalestina wanazuiliwa katika mazingira ya kutisha Israel
Oct 26, 2021 04:30Shirika moja huru la kutetea haki za binadamu limesema makumi ya wanawake wa Palestina wanashikiliwa katika mazingira ya kuogofya na yasiyo ya kibinadamu na vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika gereza la Damon.