Ansarullah: Mapambano yataendelea hadi kila shibri ya ardhi ya Yemen itakapokombolewa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i76260-ansarullah_mapambano_yataendelea_hadi_kila_shibri_ya_ardhi_ya_yemen_itakapokombolewa
Msemaji wa kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansarullah amesisitiza kuwa, mapambano dhidi ya wavamizi wa Yemen wanaoongozwa na Saudia yataendelea mpaka itakapokombolewa kila shibri ya ardhi ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 28, 2021 03:54 UTC
  • Ansarullah: Mapambano yataendelea hadi kila shibri ya ardhi ya Yemen itakapokombolewa

Msemaji wa kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen maarufu kwa jina la Ansarullah amesisitiza kuwa, mapambano dhidi ya wavamizi wa Yemen wanaoongozwa na Saudia yataendelea mpaka itakapokombolewa kila shibri ya ardhi ya nchi hiyo.

Shirika la habari la FARS limemnukuu Muhammad Abdul Salam, mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen ambaye pia ni msemaji wa harakati ya Ansarullah akionesha hisia zake baada ya vikosi vya ukombozi vya nchi hiiyo kupata ushindi mkubwa katika mkoa wa Ma'rib na kuandika: Wananchi mashujaa na waungwana wa Ma'rib, pokeeni pongezi zangu. Napenda kusisitiza kuwa, kila ardhi ya Yemen itakombolewa na kurejea chini ya kifuli ya utawala wa taifa baada ya kutimuliwa wavamizi wote.

Amesema kwa kusisitiza kwamba, inabidi mapambano ya nchi nzima ya Yemen yaendelee hadi watakapotimuliwa wavamizi katika kila shibri ya ardhi ya nchi hiyo.

Muhammad Abdul Salam

 

Vyombo mbalimbali vimetangaza habari ya ushindi mkubwa lilioupata jeshi la Yemen na harakati ya Ansarullah katika medani za mapambano za mikoa ya Ma'rib na Shabwa, kukomboewa eneo la kiistrtatijia la al Jubah na kukimbia mamluki wa wavamizi wa Yemen katika eneo la Jabal Murad kusini mwa mkoa wa Ma'rib.

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, jeshi na vikosi vya ukombozi vya wananchi wa Yemen vimepata ushindi mkubwa katika awamu mpya ya operesheni za ukombozi wa mkoa wa Ma'rib na makao yake makuu ambayo kimsingi yanahesabiwa kuwa ndio makao ya serikali ya serikali ya Abdu Rabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia Saudi Arabia.

Mkoa wa Ma'rib ni muhimu sana kutokana na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi na inatarajiwa kuwa baada ya kukombolewa mkoa huo, mamluki wa Saudia hawatakuwa tena na sehemu ya kujishikiza ndani ya ardhi ya Yemen.