-
Mawaziri wa Hizbullah na Amal watoka nje ya kikao cha baraza la mawaziri la Lebanon cha upokonyaji silaha
Sep 06, 2025 02:49Mawaziri wa Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Lebanon za Hizbullah na Amal wametoka nje ya kikao cha Baraza la Mawaziri la nchi hiyo kupinga uwepo wa kamanda wa jeshi katika kikao cha serikali cha kujadili upokonyaji silaha za Muqawama.
-
Jeshi la kizayuni laporomosha jengo la ghorofa 12 linalowapa hifadhi mamia ya Wapalestina Ghaza
Sep 05, 2025 23:36Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel siku ya Ijumaa liliripua na kuporomosha jengo la ghorofa 12 la makazi ya raia magharibi mwa Mji wa Ghaza linalowapa hifadhi mamia ya Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao katika eneo hilo lenye msongamano wa watu na ambalo limekuwa kimbilio la makumi ya maelfu ya Wapalestina.
-
Kiongozi wa Wadruze Syria amshukuru Trump, Israel na EU, asisitizia msimamo wa jamii yao kujitawala
Sep 05, 2025 23:35Kiongozi wa kiroho wa jamii ya Wadruze wa Syria, Hikmat al-Hijri ametoa shukurani kwa Marekani, utawala wa kizayuni wa Israel na nchi za Ulaya, akisisitiza kwamba haki ya kujiamualia mustakabali wao ni haki takatifu inayodhaminiwa na mikataba yote ya kimataifa.
-
Rekodi za Israel: Asilimia 75 ya Wapalestina waliokamatwa Ukanda wa Gaza ni raia
Sep 04, 2025 22:50Takriban asilimia 75 ya Wapalestina waliokamatwa na majeshi ya Israel Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro ni raia. Hii ni kwa mujibu wa data za jeshi la Israel.
-
Kiongozi wa Ansarullah asikitishwa na baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa watazamaji tu mbele ya jinai za Gaza
Sep 04, 2025 11:09Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amezungumzia jinsi watu wa Yemen wanavyodhulumiwa licha ya kuendelea kusimama kidete dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuashiria jinai za miaka miwili za utawala huo dhidi ya watu wa Gaza.
-
Smotrich atishia kufanya "mauaji ya halaiki" na kunyakuliwa kikamilifu Ukingo wa Magharibi
Sep 03, 2025 23:04Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich, ameitishia Mamlaka ya Palestina kwa "maangamizi" na kusisitiza tena wito wake wa kunyakuliwa kikamilifu eneo la Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
-
Picha za satelaiti zinaonyesha, Israel inajenga kituo kipya cha silaha za nyuklia
Sep 03, 2025 23:03Wataalamu na wachambuzi wanaamini kuwa Israel inajenga kituo kipya cha kutengeneza silaha za nyuklia, kwa mujibu wa picha za satelaiti za ujenzi unaofanyika kwa siri karibu na kinu nyuklia cha Dimona.
-
‘Majibu ya awali’: Yemen yatekeleza mashambulizi ya makombora dhidi ya Tel Aviv, uwanja wa ndege wafungwa
Sep 03, 2025 09:19Jeshi la Yemen limetekeleza mashambulizi ya makombora dhidi ya Tel Aviv, hatua iliyosababisha kufungwa kwa Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion na kuwalazimu Waisraeli kukimbilia usalama kwenye mahandaki.
-
UN: Israel imewadondoshea maguruneti askari wetu wa kulinda amani Lebanon
Sep 03, 2025 03:17Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Lebanon (UNIFIL) kimesema kuwa ndege zisizo na rubani za Israel zilidondosha maguruneti manne karibu na kambi ya walinda amani waliokuwa wakifanya kazi ya kuondoa vizuizi vya barabarani Jumanne asubuhi.
-
Watoto 43,000 wa chini ya miaka mitano Gaza wanataabika kwa utapiamlo
Sep 02, 2025 23:05Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, watoto 43,000 na wanawake 55,000 wajawazito na wanaonyonyesha katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na utapiamlo.