-
Jeshi la Israel lamuua shahidi kijana Mpalestina Ukingo wa Magharibi
Jun 12, 2021 02:42Kijana Mpalestina ameuawa shahidi Ijumaa baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamejitokeza kupinga ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni.
-
Hamas: Tumetoa pigo kubwa kwa nadharia ya usalama wa Israel
Jun 11, 2021 23:42Mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema katika mapambano ya siku 12 hivi karibuni, harakati za ukombozi wa Palestina zimetoa pigo kubwa kwa nadharia ya usalama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambayo imejengeka kwa msingi kuwa utawala huo una uwezo zaidi ya wote katika eneo.
-
Kwa nini Baraza Kuu la Kisiasa Yemen limetoa masharti matatu kwa ajili ya kufanikisha mazungumzo ya amani?
Jun 11, 2021 22:22Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen limekaribisha jitihada za kukomesha mashaka na machungu ya taifa la nchi hiyo na kutangaza masharti matatu makuu kwa ajii ya mazungumzo yajayo ya kusaka amani.
-
Sheikh Qassim: Vita vya Saif al Quds vimezidisha umoja wa wanamapambano Palestina
Jun 11, 2021 22:20Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vita vya Saif al Quds (Panga la Quds) vimepelekea kuwepo umoja na mshikamano wa muqawama kote Palestina.
-
Wananchi Bahrain waandamana kulaani kifo cha mfungwa wa kisiasa gerezani
Jun 11, 2021 08:00Mamia ya Wabahraini wamejitokeza kuandamana katika mji mkuu Manama, kumkumbuka mfungwa wa kisiasa ambaye amefariki dunia kutokana na COVID-19 akiwa katika gereza la kuogofya la utawala wa kiimla wa Aal Khalifa.
-
Ansarullah: Marekani inafadhilisha vita Yemen, haitaki amani
Jun 11, 2021 03:25Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani hatua ya Marekani ya kuliwekea vikwazo vipya taifa hilo la Kiarabu na kusisitiza kuwa, Washington inafadhilisha vita nchini Yemen, na wala haitaki amani kama inavyodai.
-
Hamas yapongeza mapambano ya jana ya Wapalestina dhidi ya Wazayuni huko Jenin
Jun 10, 2021 21:42Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amepongeza mapambano ya jana ya askari usalama wa Palestina dhidi ya wanajeshi wa utawala vamizi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi na kuyataja kuwa ni hatua ya kishujaa.
-
Jumuiya za kutetea haki za binadamu zaitaka Saudia ifute hukumu ya kifo dhidi ya al-Darwish
Jun 10, 2021 21:36Jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu zimekosoa mfumo wa mahakama za Saudi Arabia zikiitaka nchi hiyo ifute hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya kijana mmoja wa nchi hiyo.
-
Maafisa usalama 3 wa Palestina wauawa shahidi na jeshi la Israel
Jun 10, 2021 07:54Jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel limevamia mji wa Jenin ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuua shahidi maafisa usalama watatu wa Palestina.
-
HAMAS: Umma wa Kiislamu unapaswa kuungana kukomesha ugaidi wa Israel + Video
Jun 10, 2021 02:22Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Umma wa Kiislamu una jukumu la kuungana na kuwa kitu kimoja kama unataka kweli kukikomboa Kibla chao cha Kwanza yaani Msikiti wa al Aqsa na kukomesha jinai na ugaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.