-
Serikali ya Paestina yataka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi unaofanywa na Israel
Jun 02, 2021 23:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutekeleza majukumu yao mkabala na jinai za kila siku zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel za kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia akariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran
Jun 02, 2021 05:14Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia amekariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema Iran inaingilia masuala ya nchi za eneo la Magharibi mwa Asia na kuvuruga usalama wa eneo hilo.
-
Nchi za Magharibi ziko mbioni kuhuisha uhusiano wao wa kidiplomasia na Syria
Jun 01, 2021 22:43Baadhi ya nchi za Ulaya zimetangaza azma ya kufungua upya balozi na ofisi zao za kidiplomasia mjini Damascus karibuni hivi, siku chache baada ya Bashar al Assad kushinda muhula mwingine wa uchaguzi wa rais wa Syria.
-
Qatar: Mazungumzo na Iran kwa ajili ya kuleta maelewano katika eneo ni kitu cha udharura
Jun 01, 2021 06:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amesema kuwa Doha iko tayari kuchukua nafasi ya upatanishi baina ya madola makubwa ya eneo hili na kwamba mazungumzo na Iran kwa ajili ya kuleta maelewano katika eneo hili ni kitu cha dharura.
-
Utawala wa Kizayuni unazuia kuingizwa misaada ya kibinadamu huko Ghaza
Jun 01, 2021 06:05Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni ametishia kushadidisha zaidi mashambulizi huko Ukanda wa Ghaza iwapo eti muqawama utaendeleza mashambulizi yake na kueleza kuwa, kuingizwa misaada ya aina yoyote huko Ghaza kunategemea na kurejeshwa miili ya wanajeshi waliouliwa wa Israel katika eneo hilo.
-
HAMAS: Mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza unaelekea kuvunjika
Jun 01, 2021 03:26Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema wananchi wa Palestina wamekaribia sana kuuvunja mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza uliowekwa na utawala wa Kizayuni tokea mwaka 2007.
-
Wapalestina waandamana Ghaza wakitaka kufukuzwa Mkurugenzi wa UNRWA
May 31, 2021 22:21Maelfu ya raia wa Palestina jana waliandamana katika Ukanda wa Ghaza wakitaka kufukuzwa katika eneo hilo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA).
-
Umuhimu wa operesheni ya karibuni ya jeshi la Yemen nchini Saudi Arabia
May 31, 2021 22:18Wapiganaji wa kujitolewa wa harakati ya Ansarullah na jeshi la Yemen siku chache zilizopita walitekeleza operesheni ya aina yake ya kijeshi katika ardhi ya Saudi Arabia na kutoa kipigo kikubwa na cha kufedhehesha zaidi kwa majeshi ya nchi hiyo na washirika wake, kwa kadiri kwamba, vyombo vya habari vya Saudia vimepigwa na bumbuazi na kushindwa kuficha habari ya tukio hilo.
-
Kufunguliwa ubalozi wa Imarati huko Tel Aviv, pongezi kwa Israel kwa mauaji yake dhidi ya watoto wa Gaza
May 31, 2021 07:21Serikali ya Imarati jana tarehe 30 Mei ilifungua rasmi ubalozi wake mjini Tel Aviv.
-
Misri yauonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Ukanda wa Ghaza
May 31, 2021 02:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, usiku wa kuamkia leo ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu hatari za kuvunja makubaliano ya kusimamisha vita ya Ghaza.