Wapalestina waandamana Ghaza wakitaka kufukuzwa Mkurugenzi wa UNRWA
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70764-wapalestina_waandamana_ghaza_wakitaka_kufukuzwa_mkurugenzi_wa_unrwa
Maelfu ya raia wa Palestina jana waliandamana katika Ukanda wa Ghaza wakitaka kufukuzwa katika eneo hilo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2021 22:21 UTC
  • Wapalestina waandamana Ghaza wakitaka kufukuzwa Mkurugenzi wa UNRWA

Maelfu ya raia wa Palestina jana waliandamana katika Ukanda wa Ghaza wakitaka kufukuzwa katika eneo hilo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya Kibinadamu kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA).

Wapalestina hao  walifanya maandamano huku wakipiga nara za kulaani matamshi ya Matthias Schmale Mkurugenzi wa Shirika la UNRWA katika Ukanda wa Ghaza. Aidha waametaka kufukuzwa Mkurugenzi huyo. 

Matthias Schmale, Mkurugenzi wa Shirika la UNRWA Ghaza 

Katika matamshi yake ya karibuni kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, Matthias Schmale hakulaani mauaji ya raia wa Palestina yaliyofanywa na Israel bali pia alijaribu kuhalalisha mauaji hayo. Amir al Mis'hal Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi wa UNRWA huko Ghaza amesisitiza kuwa, matamshi ya Matthias Schmale yamewakwaza na kupingwa na raia wa Palestina.

Ameongeza kuwa, kusita kutoa huduma Naibu Mkurugenzi wa UNRWA huko Ghaza katika mashambulizi ya karibuni katika eneo hilo pia kunadhihirisha kuwa, maafisa hao wa UN hawako pamoja na wananchi wa Palestina katika maafa yaliyowakumba na kwa msingi huo Jumuiya ya Wfanyakazi wa UNRWA inawataka maafisa hao wa Umoja wa Mataifa kujiuzulu mara moja. 

Wapalestina 253 wameuawa shahidi katika vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Ghaza mwezi Mei mwaka huu. Watoto 66, wanawake 39 na wazee 17 ni miongoni mwa raia wa Palestina waliouliwa shahidi katika vita hivyo vya Israel. Wapalestina wengine zaidi ya 1900 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo ya kinyama dhidi ya Ghaza.