-
Jihad Islami yampongeza Ayatullah Khamenei kwa ushindi dhidi ya Wazayuni
May 22, 2021 22:19Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amemtumia barua Kiongozii Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei akiishukuru Jamhurii ya Kiislamu ya Iran kwa misaada na himaya yake katika vita vya siku 12 na utawala wa Kizayuni wa Israeil na kumpongeza kwa ushindi wa wanamapambano wa Palestina katika vita hivyo.
-
Israel imepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 2 katika vya Gaza
May 22, 2021 12:09Vita vya siku 12 vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vimesababisha hasara kubwa ya kiuchumi hasa kwa Israel.
-
Hania: Mashahidi wa Palestina wamethibitisha kuwa Quds ni mstari mwekundu
May 22, 2021 02:08Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amegusia jinsi Wapalestina walivyouliwa shahidi na Wazayuni katika vita vya Quds na kusisitiza kuwa, mashahidi hao wamewathibitisha watu wote kwamba Quds na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa taifa hilo na umma wote wa Kiislamu.
-
Wazayuni wazidi kupapurana, sasa mawaziri wawashambulia majenerali wa kijeshi kuhusu Ghaza
May 22, 2021 02:04Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni limelilaumu jeshi la utawala huo kwa kuboronga katika vita vilivyoisha juzi usiku vya Ukanda wa Ghaza.
-
Middle East Eye: Wapalestina wameungana zaidi kuliko wakati wowote mwingine
May 21, 2021 22:00Mtandao wa habari wa Middle East Eye umeandika kuwa, matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina yameonesha mshikamano na umoja usio na kifani baina ya Wapalestina kuliko wakati wowote mwingine, si ndani ya ardhi za Palestina pekee bali pia kote duniani.
-
Baada ya kula kipigo Israel, Yair Lapid asema, siku za Netanyahu zinahesabika
May 21, 2021 08:28Yair Lapid aliyepewa jukumu la kuunda serikali ya utawala wa Kizayuni amekiri kwamba Wazayuni hawakupata matunda yoyote katika vita vya siku 11 vilivyoisha jana usiku na kusisitiza kuwa, wakati wa kuondoka Benjamin Netanyahu umewadia.
-
Baada ya kushindwa Ghaza, sasa Wazayuni walana wao kwa wao
May 21, 2021 07:49Baada ya kushindwa katika vita vya siku 11 baina yao na wanamapambano wa Palestina, sasa wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamenza kupapurana wao kwa wao.
-
Palestina kuushitaki utawala wa Kizayuni katika mahakama ya ICC
May 21, 2021 07:44Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani wa Palestina amesema kuwa, mamlaka hiyo itaishitaki Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, kwa jinai zake za kuua watoto wadogo na wanawake wa Wapalestina wasio na hatia.
-
Hizbullah: Vita vya "Seif al-Quds" vimeonyesha kuwa, Israel ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui
May 21, 2021 03:46Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, vita vya "Seif al-Quds" vimeonyesha kuwa, utawala haramu wa Israel ni dhaifu kuliko hata nyumba ya buibui.
-
Hatimaye vita vyasitishwa Gaza baada ya Israel kukubali mpango wa kusitisha vita
May 20, 2021 23:24Baada ya siku 11 za hujuma na mashambulio ya kijeshi ya utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel hatimaye utawala huo umeafiki mpango wa kusitisha vita.