Middle East Eye: Wapalestina wameungana zaidi kuliko wakati wowote mwingine
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70408-middle_east_eye_wapalestina_wameungana_zaidi_kuliko_wakati_wowote_mwingine
Mtandao wa habari wa Middle East Eye umeandika kuwa, matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina yameonesha mshikamano na umoja usio na kifani baina ya Wapalestina kuliko wakati wowote mwingine, si ndani ya ardhi za Palestina pekee bali pia kote duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 21, 2021 22:00 UTC
  • Middle East Eye: Wapalestina wameungana zaidi kuliko wakati wowote mwingine

Mtandao wa habari wa Middle East Eye umeandika kuwa, matukio ya karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina yameonesha mshikamano na umoja usio na kifani baina ya Wapalestina kuliko wakati wowote mwingine, si ndani ya ardhi za Palestina pekee bali pia kote duniani.

Mtandao wa habari wa Middle East Eye umesema kuwa, mapigano ya karibuni baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamapambano wa Palestina yamepelekea kuibuka umoja na mshikamano usio na kifani baina ya matabaka mbalimbali ya Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi, Gaza, maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel na kote duniani. 

Kituo hicho chenye makao yake London nchini Uingereza kimeeleza kuwa, kinyume chake, jamii ya Wazayuni imeonekana kukosa ushirikiano na uwiano katika matendo kuliko wakati wowote mwingine, na stratejia ya "kuzusha tofauti baina ya watu na kisha kuwadhibiti" ya Israel inaelekea kusambaratika. 

Maroketi ya wanamapambano wa Palestina yakivurumushwa dhidi ya Israel

Ripoti ya Middle East Eye ienukuu matamshi ya mhariri mkuu wa gazeti la Kizayuni la Haaretz akisema kuwa, mashambulizi ya sasa ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa kwa miaka mingi ndiyo operesheni mbaya zaidi ya kijeshi katika mtazamo wa mipango na utayarifu. 

Mapigano baina ya wanamapambano wa Palestina na utawala wa kikatili wa Israel yalianza tarehe 10 Mei baada ya kumalizika muhula uliokuwa umetangazwa na wapigania uhuru wa Palestina wakiitaka Israel ikomeshe uvamizi wake katika mji wa Quds na Msikiti wa al Aqsa. 

Usiku wa kuamkia Ijumaa ya jana utawala wa kigaidi wa Israel ulitangaza usitishwaji vita na Wapalestina.