Jihad Islami yampongeza Ayatullah Khamenei kwa ushindi dhidi ya Wazayuni
Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amemtumia barua Kiongozii Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei akiishukuru Jamhurii ya Kiislamu ya Iran kwa misaada na himaya yake katika vita vya siku 12 na utawala wa Kizayuni wa Israeil na kumpongeza kwa ushindi wa wanamapambano wa Palestina katika vita hivyo.
Sehemu moja ya barua hiyo ya Ziad Al-Nakhaleh iliyochapishwa jana Jumamosi imesema kuwa: Kwa fahari kubwa na kwa niaba yangu mwenyewe na ndugu zangu katika komandi na wapiganaji wa harakati ya Jihad Islami na Batalioni ya Qud, napenda kukupongeza kwa ushindi wa taifa la Palestina na wanamapambano shupavu dhidi ya adui Mzayuni na ubeberu na uovu wa utawala huo.
Al-Nakhaleh ameongeza kuwa: "Himaya ya misaada yako ya kudumu katika nyanja zote imekuwa na nafasi na mchango mkubwa zaidi katika mapigano ya "Panga la Quds" na mafanikio yake. Wanamapambano wa Kipalestina, wamesimama kidete na kwa ushujaa mkubwa katika medani ya vita licha ya nguvu kubwa ya kijeshi ya adui."
Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami amesema: "Taifa na wanamapambano wa Palestina wameiviringisha pua ya adui kwenye ugongo katika mapigano yaliyowafurahisha waumini kote duniani na kudhihirisha tena kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel ni dhaifu sana kuliko hata tando za buibui. Katika kipindi hiki cha kihistoria tunakushukuru wewe na ndugu zetu katika Kikosi cha Quds kwa kuwa pamoja nasi kwa miaka mingi na kutupa misaada na ujuzi wenu kwa ikhasi isiyo na kifani hadi tumeweza kupata ushindi katika siku kama hii."
Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami amesema: "Naona lazima kumkumbuka shahidi kipenzi na kamanda mpendwa wetu Haj Qassem Soleimani ambaye amepata daraja ya juu ya kuuliwa shahidi. Tunamkumbuka na kumhisi zaidi Kamanda Soleimani katika nyakati hizi za kihistoria."