-
Pigo la kiusalama kwa Israel, ngao yake ya makombora ya 'Kuba la Chuma' yafeli
Apr 25, 2021 21:58Katika siku za Jumatano na Alkhamisi wiki iliyopita, kulijiri matukio mawili ya kiusalama katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimpeachikwa jina bandia la Israel. Matukio hayo yaliweka wazi udhaifu mkubwa wa kiusalama, kijeshi, na kijasusi wa utawala wa wa Kizayuni wa Israel.
-
Yafichuka: Bin Salman anahonga vyombo vya habari ili kusafisha sura yake duniani
Apr 25, 2021 07:49Mtandao mmoja wa habari nchini Marekani umefichua kuwa, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman amefunga mkataba wa gharama kubwa ya fedha na kampuni moja ya Marekani kwa shabaha ya kuboresha sura yake iliyochafuka sana mbele ya macho ya walimwengu.
-
Rais Barham Salih wa Iraq aamuru uchunguzi mlipuko wa hospitali ya wagonjwa wa corona, makumi wamefariki dunia
Apr 25, 2021 05:01Rais Barham Salih wa Iraq ametoa amri ya kufanyika uchunguzi kuhusiana na mlipuko uliotokea mapema leo katika Hospitali ya Ibn Khatib mjini Baghdad iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa corona. Makumi ya wagonjwa wameuawa katika ajali hiyo.
-
Jeshi la Yemen lashambulia kwa droni kituo cha kijeshi cha Saudia mkoani Asir
Apr 25, 2021 03:24Vikosi vya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi vimefanya shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa kijeshi wa Asir, kusini magharibi mwa Saudi Arabia kwa kutumia ndege isiyo na rubani.
-
Moto waua watu 55 katika hospitali ya wagonjwa wa corona mjini Baghdad, Iraq
Apr 24, 2021 22:52Watu wasiopungua 55 wameaga dunia katika ajali ya moto iliyosababishwa na kuripuka mitungi ya oksijini kwenye hospitali moja ya wagonjwa wa corona katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
-
Jordan yataka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuwaunga mkono Wapalestina
Apr 24, 2021 22:10Serikali ya Jordan imelaani hujuma na mashambulio ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji wa Baytul-Muqaddas na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na za maana za kuiunga mkono Quds pamoja na wakazi wa mji humo mtakatifu.
-
Bahrain yaendelea kushuhudia maandamano ya kutaka kuachiliwa wafungwa wa kisiasa
Apr 24, 2021 22:10Wananchi wa Bahrain wameendelea kuandamana wakiutaka utawala wa kiimla wa nchi hiyo kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Lebanon; nchi yenye mawaziri wakuu wawili kwa wakati mmoja
Apr 24, 2021 22:08Katika miezi minane iliyopita, Lebanon imekuwa na mawaziri wakuu wawili kwa wakati mmoja. Tarehe 4 Agosti mwaka uliopita mji mkuu wa nchi hiyo Beirut, ulishuhudia mlipuko mkubwa ambao ulipelekea watu karibu 200 kupoteza maisha.
-
Makundi ya muqawama ya Palestina: Quds na msikiti wa Al Aqsa ni mstari mwekundu
Apr 24, 2021 08:36Kitengo cha pamoja cha makundi ya muqawama ya Palestina kimetangaza kuwa, Quds na msikiti wa Al Aqsa ni mstari mwekundu; na uamuzi wa mwisho kuhusu matukufu mawili hayo utaamuliwa na muqawama.
-
Serikali ya Saudia yabomoa msikiti mwingine wa Waislamu wa Kishia
Apr 24, 2021 08:08Mabuldoza ya utawala wa Aal Saud yamebomoa msikiti mwingine ulioko kandokando ya mji wa Qatif ambao wakazi wake ni Waislamu wa madhehebu ya Shia mashariki ya Saudi Arabia.