-
Shirika la WFP: Yemen inajongewa na ukame mbaya zaidi wa karne
Mar 13, 2021 09:34Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ametahadharisha kuwa, Yemen inakaribia kukumbwa na ukame mbaya zaidi wa karne na kueleza kwamba, watu milioni 16 nchini humo wanataabika kwa njaa huku milioni tano kati yao wakikabiliwa na hatari ya kukumbwa na ukame.
-
Israel ina hofu ya HAMAS kushinda uchaguzi wa Palestina na kudhibiti pia Ufukwe wa Magharibi
Mar 13, 2021 04:27Wachambuzi wa mambo katika duru za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamesema mashirika ya usalama ya utawala huo yana hofu na wasiwasi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kushinda uchaguzi ujao na kulidhibiti pia eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Abbas amshukuru Ayatullah Sistani kwa msimamo wa kuihami na kuitetea Palestina
Mar 13, 2021 03:46Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemwandikia barua Ayatullah Ali Sistani kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq kumpongeza na kumshukuru kwa misimamo yake ya kuitetea na kuihami Palestina katika mkutano wake na Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.
-
Nchi za Ulaya na Marekani zakasirishwa na oparesheni ya kuukomboa mji wa Maarib huko Yemen
Mar 12, 2021 23:07Nchi nne za Ulaya pamoja na Marekani zimetoa taarifa ya pamoja zikilaani oparesheni ya kuukomboa mji wa Maarib huko Yemen na zimetaka kusimamishwa oparesheni hiyo.
-
Lavrov: Lengo la kikao cha Afghanistan huko Russia ni kusaidia mazungumzo kati ya Waafghani huko Qatar
Mar 12, 2021 23:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, mazungumzo ya amani ya Afghanistan huko Moscow mji mkuu wa Russia si kwa ajili ya kuyashindanisha na mazungumzo ya makundi ya Kiafghani huko Qatar ; bali yatafanyika kwa ajili ya kusaidia mchakato huo.
-
Mayahudi 300 wa Ethiopia (Mafalasha) wawasili Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni
Mar 12, 2021 08:33Utawala wa Kizayuni wa Israel umewahamishia katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, Mayahudi wengine 300 wa Ethiopia ambao ni maarufu kwa jina la Mafalasha, ikiwa ni sehemu ya njama za kiuadui za Wazayuni, za kuvuruga muundo wa kijamii wa Palestina.
-
Bunge la Ulaya lalaani ukiukwaji wa haki za binadamu Bahrain
Mar 12, 2021 04:51Bunge la Umoja wa Ulaya limepasisha azimio ambalo limeitaka Bahrain isitishe mara moja ukandamizaji wa haki za binadamu za wanaharakati na wafungwa wa kiitikadi nchini humo.
-
Jordan yasisitiza Israel haipaswi kuingilia mambo ya ndani ya Msikiti wa Al Aqsa
Mar 12, 2021 04:49Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan imesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel haupaswi kuingilia mambo ya Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa sababu Wazayuni hawana mamlaka yoyote katika eneo hilo takatifu.
-
Mawaziri wa Qatar, Ururuki na Russia waeleza msimamo wa nchi zao kuhusu Syria
Mar 11, 2021 09:23Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki, Russia na Qatar leo wameshiriki katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huko Doha mjini mkuu wa Qatar na kubainisha msimamo wa nchi zao kuhusiana na matukio ya Syria.
-
Mrithi wa ufalme wa Saudia yuko tayari kwenda UAE kukutana na waziri mkuu wa Israel
Mar 11, 2021 03:48Duru za kuaminika katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimeripoti kuwa, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Mohammad bin Salman yuko tayari kukutana na waziri mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wakati kiongozi huyo wa Kizayuni atakapokuwa safarini huko Abu Dhabi.