Bunge la Ulaya lalaani ukiukwaji wa haki za binadamu Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i67796-bunge_la_ulaya_lalaani_ukiukwaji_wa_haki_za_binadamu_bahrain
Bunge la Umoja wa Ulaya limepasisha azimio ambalo limeitaka Bahrain isitishe mara moja ukandamizaji wa haki za binadamu za wanaharakati na wafungwa wa kiitikadi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 12, 2021 04:51 UTC
  • Bunge la Ulaya lalaani ukiukwaji wa haki za binadamu Bahrain

Bunge la Umoja wa Ulaya limepasisha azimio ambalo limeitaka Bahrain isitishe mara moja ukandamizaji wa haki za binadamu za wanaharakati na wafungwa wa kiitikadi nchini humo.

Azimio hilo lilipitishwa kwa wingi wa kura Alhamisi ambapo wabunge 633 waliunga mkono 11 walipinga na 45 walijizuia kupiga kura.

Aidha azimio hilo limesema hali ya haki za binadamu inaendelea kuwa mbaya nchini Bahrain hasa baada ya ufalme huo kuanza kukabiliwa na mwamko wa wananchi wanaopinga ukandamizaji.

Wabunge hao wa Ulaya ameangazia kadhia ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa nchini Bahrain na kusema kuna dosari nyingi katika kesi zao na uadilifu haujatendeka.

Maandamano dhidi ya mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa

Mwamko wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 mwaka 2011, na ungali unaendelea licha ya utawala huo dhalimu kushadidisha ukandamizaji na utumiaji mabavu dhidi ya wananchi hao wanaotaka mabadiliko.

Tokea Februari 14 mwaka 2011 hadi sasa utawala wa Aal Khalifa umewakamata na kuwafunga jela zaidi ya raia 11,000 kwa visingizio mbali mbali visivyo na maana.