-
HAMAS yasisitizia umoja wa Wapalestina mkabala wa njama za Israel-Marekani
Sep 04, 2020 02:37Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya kwa mara nyingine tena amesisitiza udharura wa kuungana na kushirikiana makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Palestina kwa lengo kuzima njama za maadui zao, yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na baadhi ya tawala za kizandiki za Kiarabu.
-
Arab League yawaacha mkono Wapalestina na kuunga mkono mapatano ya UAE na Wazayuni
Sep 03, 2020 03:38Katika hatua inayoonyesha kuipiga vita na kuiacha mkono Palestina na badala yake kuunga mkono hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kufanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelikataa ombi la Palestina la kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo.
-
HAMAS yasisitiza kuendeleza uhusiano wa kistratejia na Hizbullah ya Lebanon
Sep 03, 2020 03:37Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, uhusiano wa kistratejia baina ya makundi ya ukombozi na muqawama na Hizbullah ya Lebanon utapelekea kukombolewa Palestina kutoka kwenye makucha ya maghasibu wa Israel.
-
Malengo ya safari ya Ismail Haniya nchini Lebanon baada ya kupita miaka 27
Sep 03, 2020 02:14Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, baada ya miaka 27 juzi Septemba Mosi aliwasili Beirut mji mkuu wa Lebanon.
-
Jumuiya 30 za kimataifa zataka Saudia ishinikizwe kuwaachia huru watetezi wa haki za binadamu
Sep 02, 2020 23:38Jumuiya 30 za kimataifa za kutetea haki za binadamu zikiongozwa na Human Rights Watch zimeitaka jamii ya kimataifa iishinikize Saudi Arabia ili iwaachie huru watetezi wa haki za binadamu na kusitisha ukiukaji wote wa haki za raia.
-
Jordan yatoa msimamo kuhusu njama ya UAE na Israel ya kutaka kubadilisha hali ya msikiti wa Al Aqsa
Sep 02, 2020 10:39Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan imetangaza kuwa, Idara ya Waqfu ya nchi hiyo ndio pekee yenye mamlaka na ustahiki wa kusimamia masuala ya Msikiti mtukufu wa Al Aqsa na uendeshaji wake.
-
Rais wa Ufaransa akiri: Hizbullah ni mwakilishi wa sehemu mojawapo ya wananchi wa Lebanon
Sep 01, 2020 22:11Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema, Hizbullah ni mwakilishi wa sehemu mojawapo ya wananchi wa Lebanon.
-
Akiba ya fueli al Hudaydah imemalizika, Saudia yaendelea kuzuia meli 21 za mafuta za Yemen
Sep 01, 2020 22:06Shirika la mafuta la Yemen limesema, akiba yote ya fueli ya shirika hilo iliyokuwepo katika bandari ya al Hudaydah imemalizika.
-
Waziri wa Afya wa Yemen aukosoa Umoja wa Mataifa kwa kupuuza hali ya kiafya ya nchi hiyo
Sep 01, 2020 08:05Waziri wa Afya wa Yemen amekosoa upuuzaji unaofanywa na Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa hatua zinazondelea kutekelezwa na muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia za kuzuia meli na taathira mbaya za hatua hiyo kwa hali ya kiafya ya nchi hiyo.
-
Kufanya safari tena Rais wa Ufaransa nchini Lebanon
Sep 01, 2020 06:10Baada ya kupita takriban mwezi mmoja tangu kutokea mlipuko mkubwa katika bandari ya Beirut, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa mara ya pili ameelekea nchini Lebanon.