-
Ansarullah: Kimya cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mbele ya mapatano ya Abu Dhabi-Tel Aviv kinaaibisha
Aug 17, 2020 02:16Msemaji wa harakati ya Ansarullah ya wananchi wa Yemen amesema kuwa kimya cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) mbele ya hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel ni fedheha na aibu kubwa.
-
Taathira za kiusalama za ‘makubaliano ya usaliti’ ya Israel na Imarati
Aug 17, 2020 02:08Makubaliano ya hiana na usaliti ya Imarati na utawala dhalimu wa Israel ya kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia baina yao yatakuwa na matokeo na taathira tofauti katika uga wa usalama.
-
Hamas yapinga vikali kutiwa mbaroni Sheikh Raed Salah
Aug 16, 2020 21:59Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumtia tena mbaroni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ina lengo la kuwafutilia mbali walinzi wa Msikiti wa Al Aqsa.
-
Mufti Mkuu wa Iraq atoa wito wa kuanzishwa mapambano dhidi ya uvamizi wa Marekani
Aug 16, 2020 06:59Mufti Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq ametoa wtito kwa vijana kujiandaa kwa ajili ya kuanzisha mapambano dhidi ya uvamizi wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Umoja wa Mataifa: Mazungumzo kati ya Waafghani yatafanyika wiki hii Doha Qatar
Aug 16, 2020 06:57Licha ya kuweko hitilafu kubwa kuhusiana na tarehe ya kufanyika mazungumzo baina ya Waafghani, lakini Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mazungumzo hayo yatafanyika wiki hii katika mji mkuu waQatar Doha.
-
UAE: Hakuna hakikisho lolote la kughairishwa umegaji wa eneo la Ufukwe wa Magharibi
Aug 15, 2020 21:46Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Imarati (UAE) amekiri kuwa hakuna hakikisho lolote lililotolewa katika makubaliano kati ya nchi hiyo na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel la kufutwa mpango wa kulimega eneo la ardhi ya Palestina la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Makumi ya waitifaki wa Saudia waangamizwa katika shambulio mkoani Maʼrib
Aug 15, 2020 06:35Mlipuko uliotokea katika mkoa wa Maʼrib huko katikati mwa Yemen umeangamiza makumi ya mamluki na waitifaki wa Saudi Arabia.
-
Nukta tano muhimu katika hotuba ya Sayyid Hassan Nasrallah katika mwaka wa 14 wa ushindi wa Vita vya Siku 33
Aug 15, 2020 05:16Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Ijumaa usiku alizungumza kwa mnasaba wa mwaka wa 14 wa ushindi wa harakati hiyo ya muqawama katika Vita vya Siku 33 vya Mwaka 2006.
-
Sayyid Hassan Nasrullah: Kuhuishwa uhusiano kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni ni huduma ya uchaguzi kwa Trump na Netanyahu
Aug 15, 2020 03:15Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon jana usiku alihutubu kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka 14 wa ushindi wa muqawama katika vita vya siku 33 na kueleza kuwa, kuhuishwa uhusiano kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni ni huduma ya uchaguzi kwa Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni.
-
Muungano wa Maulama wa Kiislamu: Hatua ya Imarati kuanzisha uhusiano na Israel ni usaliti mkubwa
Aug 14, 2020 22:28Jumuiya ya Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu imelaani makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Imarati na utawala haramu wa Israel yaliyofikiwa kwa upatanishi wa Marekani.