-
Waitifaki wa Saudia na Imarati waendelea kutwangana risasi na kuuana nchini Yemen
Jul 15, 2020 09:24Mapigano kati ya wanamgambo wa Baraza la Mpito linaloungwa mkono na Imarati na wale wanaoungwa mkono na Saudi Arabia katika mkoa wa Abyan kusini mwa Yemen yameshtadi na kupamba moto.
-
Zarif: Mzingiro wa Yemen katika kipindi hiki cha corona haukubaliki
Jul 14, 2020 08:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya Saudi Arabia na washirika wake ya kuendelea kuizingira Yemen na kutwaa meli zinazobeba misaada ya kibinadamu na nishati kwa ajili ya watu wa nchi hiyo katika kipindi hiki cha maambukizi ya corona, haikubaliki.
-
Russia: Misaada ya kibinadamu nchini Syria haipaswi kuwekewa masharti ya kisiasa
Jul 14, 2020 06:41Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Syria haipaswi kuhusishwa na masuala ya kisiasa na kuzusha wasiwasi kwa baadhi ya watu.
-
UN yasikitishwa na mashambulizi ya Saudia yaliyoua watoto 7, wanawake 2 Yemen
Jul 14, 2020 03:42Umoja wa Mataifa umethibitisha habari ya kuuawa watoto wadogo saba na wanawake wawili katika mashambulizi ya anga yaliyolenga makazi ya raia huko kaskazini magharibi mwa Yemen.
-
Mawaziri wa EU: Mwanya wa kuzuia uporaji wa ardhi za Wapalestina unazidi kuwa finyu
Jul 14, 2020 03:40Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wametoa mwito kwa EU-mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Israel-kuchukua hatua za makusudi na haraka kuzuia mpango wa Tel Aviv wa kutwaa ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Ansarullah ya Yemen na kubakia hatua moja tu kabla ya kuukomboa mji wa kistratejia wa Ma'rib
Jul 14, 2020 02:50Brigedia Jenerali Abdullah Yahya al-Hakim, mkuu wa intelijensia wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen ametangaza kuwa, mji wa Ma'rib ulioko katikati mwa nchi hiyo unakaribia kukombolewa kutoka kwenye makucha ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Jumuiya ya Mateka wa Palestina: Madaktari wa kimataifa wachunguze jela za Israel
Jul 13, 2020 22:02Jumuiya ya Mateka wa Palestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala haramu wa Israel imetoa wito wa kupelekwa madaktari wa kimataifa katika jela za Israel ili kufuatilia hali ya mateka wa Kipalestina katika kipindi hiki cha kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.
-
Wayemen walipiza kisasi kwa kupiga kwa makombora maeneo ya Saudia
Jul 13, 2020 03:01Duru za Saudi Arabia mapema leo asubuhi zimetangaza habari ya kusikika sauti za miripuko kadhaa katika maeneo ya Khamis Mushait na Abha ya kusini mwa nchi hiyo.
-
Televisheni ya Saudia yaeneza uongo na kuendesha propanda chafu dhidi ya Wapalestina
Jul 13, 2020 02:57Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Ukanda wa Ghaza imeilalamikia vikali televisheni ya Saudi Arabia ya al Arabia kwa kueneza uongo na propaganda chafu dhidi ya Wapalestina na imekanusha madai ya uongo ya televisheni hiyo iliyodai kuwa baadhi ya makamanda wa muqawama wa Palestina wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Maandamano mtawalia dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Jul 12, 2020 23:38Ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa mara ya kadhaa zimeshuhudia maandamano mtawalia ya wananchi katika kipindi cha miezi miwili ya hivi karibuni dhidi ya Baraza la Mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.