Russia: Misaada ya kibinadamu nchini Syria haipaswi kuwekewa masharti ya kisiasa
-
Sergey Vershinin
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Syria haipaswi kuhusishwa na masuala ya kisiasa na kuzusha wasiwasi kwa baadhi ya watu.
Sergey Vershinin amesema kuwa, misaada yote ya kibinadami inapaswa kupelekwa Syria baada ya kufanya uratibu na kwa kushirikiana na serikali halali ya nchi hiyo.
Vershinin ameitaja hatua ya serikali ya Syria ya kutuma misaada ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuwa ni yenye mafanikio na amezitaka pande zote kuendelea kutuma misaada ya kibinadamu kwa watu wote wa Syria kwa kuzingatia na kuheshimu sheria za kimataifa.
Marekani na washirika wake wa Kimagharibi wanafanya jitihada za kutumia vibaya misaada ya kibinadamu ya kimataifa inayopelekwa Syria kwa maslahi yao ya kisiasa, suala ambalo limepingwa vikali na serikali ya Damascas na washirika wake.
Siku chache zilizopita pia Russia na China zimelipigia kura ya veto azimio lililotaka kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa nchini Syria bila ya idhini wala kushauriana na serikali kuu ya nchi hiyo. Moscow na Beijing zinasema maazimio kama hayo yanakiuka mamlaka ya kujitawala Syria na yanatumisa kwsa malngo ya kisiasa.
Mgogoro nchini Syria ulianza mwaka 2011 kwa hujuma na mashambulio makali ya makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa na Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao kwa lengo la kubadilisha mlingano wa nguvu katika eneo la magharibi mwa Asia kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Hata hivyo kwa msaada wa washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uungaji mkono wa Russia, jeshi la Syria limefanikiwa kulisambaratisha kundi la kigaidi la DAESH nchini humo.