-
Hamas yalaani hatua ya Wazayuni ya kubomoa vituo vya Wapalestina
Jun 17, 2020 22:22Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kubomoa vituo vya Wapalestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu ni jitihada za utawala huo zinazolenga kubadili utambulisho wa Quds; njama ambazo hazitafikia popote.
-
Bahrain; hukumu mbili za kifo katika siku moja
Jun 16, 2020 22:08Mahakama ya juu ya Bahrain tarehe 15 Julai ilitoa hukumu ya kunyongwa vijana wawili wa nchi hiyo kwa kutegemea ushahidi bandia
-
Ansarullah nayo yauponda Umoja wa Mataifa, yakosoa kuondolewa Saudia katika 'orodha ya fedheha'
Jun 16, 2020 08:28Harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah imeutaka Umoja wa Mataifa kutupilia mbali uamuzi wake wa kuliondoa jina la Saudi Arabia na washirika wake katika orodha ya makundi yanayokanyaga na kuvunja haki za watoto.
-
Guterres akosolewa kwa kuiondoa Saudia katika 'orodha ya fedheha'
Jun 16, 2020 03:36Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamemjia juu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa kuuondoa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika orodha ya makundi yanayokanyaga haki za watoto.
-
Imarati, mhandisi wa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na nchi za Kiarabu
Jun 16, 2020 01:14Yousef al Otaiba, balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mjini Washington, Marekani amesema katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth kwamba anaunga mkono kuweko uhusiano wa kawaida baina ya Abu Dhabi na utawala wa Kizayuni na kwamba Israel inaweza kuifanya Imarati kuwa lango la kuingilia kwenye nchi za eneo hili na dunia nzima kiujumla.
-
UN: Athari za corona kuua watoto 50,000 Afrika Kaskazini na Asia Magharibi
Jun 15, 2020 10:40Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, yumkini athari za ugonjwa wa COVID-19 zikaua makumi ya maelfu ya watoto katika nchi za kaskazini mwa Afrika na Asia Magharibi.
-
Israel kujenga 'vitongoji 300 vya Trump' katika Milima ya Golan, Syria
Jun 15, 2020 02:23Utawala ghasibu wa Israel unapanga kujenga mamia ya vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika Miinuko ya Golan nchini Syria, vitakavyoitwa "Miinuko ya Trump".
-
Hamas yataka wanazuoni wa Kiislamu waunde kamati ya kuzima njama za Israel
Jun 14, 2020 22:41Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa mwito kwa wanazuoni wa Kiislamu kuunda kamati ya uratibu itakayopewa jukumu la kuunda na kutekeleza mpango wa kistratajia wa kuunga mkono kadhia ya Palestina na kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel na Rais Donald Trump wa Marekani zilizopewa jina la "Muamala wa Karne."
-
Madaktari wasio na mipaka watahadharisha kuhusu kusambaratika mfumo wa afya na tiba Yemen
Jun 14, 2020 06:02Mkuu wa wahudumu wa Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) huko Yemen amesema kuwa hali ya kiafya na kitiba katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita imezidi kuwa ya hatari kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
-
Palestina yataka kikao cha Baraza la Usalama kijadili Israel kughusubu Ukingo wa Magharibi
Jun 14, 2020 03:38Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametoa wito wa kikao kijacho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kifanyike katika ngazi ya juu itakayojumuisha mawaziri wa mambo ya nje badala ya wawakilishi wakati wa kujadiliwa mpango tata wa Israel wa kuteka na kughusubu maeneo zaidi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.