-
Malengo ya Saudi Arabia ya kukanyaga mara kwa mara usitishaji vita nchini Yemen
Apr 13, 2020 01:41Habari kutoka Yemen zinasema kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa kiimla wa Saudi Arabia ungali unaendelea kukanyaga usitishaji vita uliotangazwa na muungano huo wenyewe huko Yemen.
-
Mashambulio ya Saudia yameisababishia sekta ya elimu Yemen hasara ya mabilioni
Apr 12, 2020 23:09Wizara ya Elimu ya Yemen imesema mashambulio na hujuma zinazofanywa na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu zimeisababishia sekta ya elimu ya nchi hiyo hasara ya dola bilioni 12.
-
UAE yanunua mfumo wa makombora wa Israel na kuwapa wapiganaji wa Haftar
Apr 12, 2020 23:08Umoja wa Falme za Kiarabu umenunua mfumo wa kisasa wa makombora kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa ajili ya kuwapa wanamgambo wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar.
-
Saudia inaongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa Corona katika nchi za Kiarabu
Apr 12, 2020 23:06Saudi Arabia inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na waathirika wengi wa virusi vya Corona kati ya nchi za Kiarabu, baada ya kufikisha waathirika zaidi ya 4000.
-
Kushtadi mashambulizi ya mizinga ya jeshi la Uturuki kaskazini mwa Syria
Apr 12, 2020 22:23Uvamizi wa jeshi la Uturuki katika maeneo ya kaskazini mwa Syria, bado unaendelea na katika uwanja huo vyombo vya habari vya Uturuki vimethibitisha kuendelea mashambulizi ya mizinga ya askari wa nchi hiyo ndani ya maeneo ya taifa hilo la Kiarabu.
-
Bunge la Jordan: Mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel waachiliwe huru
Apr 12, 2020 07:47Bunge la Jordan limetoa wito wa kuachiliwa huru mateka wote wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya kutisha ya utawala haramu wa Israel.
-
Al Houthi: Majukumu halisi ya usitishaji vita Yemen yanapaswa kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa
Apr 12, 2020 03:09Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema majukumu ya nchi vamizi huko Yemen kwa jaili ya kusitisha vita yanapaswa kubainishwa na kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
-
Mwanaharakati ataka kufanyike uchunguzi kuhusu misaada ya Trump kwa Israel licha ya Marekani kulemewa na virusi vya corona
Apr 11, 2020 23:53Mwanaharakati mashuhuri wa Marekani, Ariel Gold amezungumzia haja kubwa ya wafanyakazi wa sekta ya afya na tiba katika hospitali za nchi hiyo kwa vifaa na zana za tiba kama barakoa na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu shehena ya zawadi za barakoa iliyotumwa na Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo huko Israel.
-
HRW yaitaka serikali ya India kufuta sheria mpya ya uraia inayowabagua Waislamu
Apr 11, 2020 23:53Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya India ifutilie mbali sheria mpya ya uraia inayowabagua Waislamu kwa misingi ya dini yao.
-
Saudia na Imarati zinafanya njama ya kueneza corona nchini Yemen
Apr 11, 2020 23:52Naibu Mkuu wa Ofisi ya Utendaji ya harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema kuwa, mpango wa usitishaji vita uliopendekezwa na Saudi Arabia ni hadaa na kwamba Riyadh na wavamizi wenzake dhidi ya Yemen hawatekelezi mpango huo.