-
Waziri kivuli wa Mambo ya nje Uingereza: Mauaji ya Khashoggi bado hayajasahaulika
Apr 02, 2020 22:29Waziri kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesisitiza kwamba licha ya kuenea maambukizi ya virusi vya Corona, lakini suala la mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Aal Saud bado halijasahaulika.
-
Waziri wa Afya wa Israel, mkewe wapatwa na virusi vya corona
Apr 02, 2020 09:07Waziri wa Afya wa Israel Yaakov Litzman na mke wake wamepatwa na virusi vya corona na wamewekwa karantini.
-
Kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina bila kujali maambukizi ya virusi vya corona
Apr 02, 2020 08:11Mripuko wa maambukizo ya kirusi cha corona cha covid-19 umesambaa Palestina na katika ardhi zake zingine zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel huku utawala huo haramu wa Kizayuni ukiwa unaendeleza jinai zake dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Netanyahu afedheheka akitaka kuchafua sura ya Iran
Apr 02, 2020 03:05Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu hivi karibuni alionyesha mkanda wa video akidai kuwa unaonyesha jinsi Iran inavyowatupa na kuwazika wahanga wa virusi vya corona jalalani, lakini baadaye kidogo imedhihiri kwamba mkanda huo wa video ni sehemu ya sinema iliyoonyeshwa kwenye televisheni nchini Marekani mwaka 2007.
-
Saudia yapeleka maski zenye virusi vya corona nchini Yemen
Apr 01, 2020 21:57Waziri wa Habari wa Yemen amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba ndege za kivita za muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia zimedondosha maski (barakoa) zenye virusi vya corona katika miji mbalimbali ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu.
-
Saudi Arabia yakiuka usitishaji vita al-Hudaydah mara 108 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita
Apr 01, 2020 07:48Kanali ya Televisheni ya al-Masirah imetangaza kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya Yemen imekiuka mara 108 makubaliano ya usitishaji al-Hudaydah katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
-
Saudia yawataka Waislamu kuchelewesha maandalizi ya ibada ya Hija kutokana na kasi ya corona
Apr 01, 2020 03:39Waziri wa Hija wa Saudi Arabia amewataka Waislamu kote duniani kuchelewesha maandalizi ya ibada ya mwaka huu ya Hija hadi pale hali ya mambo kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona duniani itakapobaika vyema.
-
Mousavi: Harakati za Marekani nchini Iraq zinasababisha ghasia na ukosefu wa amani
Apr 01, 2020 03:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria harakati za wanajeshi wa Marekani huko Iraq na kueleza kuwa, harakati hizo mbali na kukiuka mamlaka ya kitaifa ya Iraq zinasababisha ghasia na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi.
-
Siku ya Ardhi Palestina; miaka 44 baada ya jinai za Israel za mwaka 1976
Mar 31, 2020 08:59Jumatatu ya jana tarehe 30 Machi ilisadifiana na mwaka wa 44 wa Yaumul Ardh (Siku ya Ardhi) huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Tarehe 30 Machi mwaka 1976, viongozi wa utawala ghasibu wa Israel walipora maelfu ya hekari za ardhi za Wapalestina katika eneo la al-Khalil lililopo kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Trump azikosoa Saudi Arabia na Russia kwa kuvuruga soko la mafuta
Mar 31, 2020 02:29Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kuzikosoa Saudi Arabia na Russia kutokana na kuvuruga soko la mafuta, amesema kuwa Riyadh na Moscow zimepatwa na wendawazimu katika suala hilo.