Trump azikosoa Saudi Arabia na Russia kwa kuvuruga soko la mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60079-trump_azikosoa_saudi_arabia_na_russia_kwa_kuvuruga_soko_la_mafuta
Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kuzikosoa Saudi Arabia na Russia kutokana na kuvuruga soko la mafuta, amesema kuwa Riyadh na Moscow zimepatwa na wendawazimu katika suala hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 31, 2020 02:29 UTC
  • Trump azikosoa Saudi Arabia na Russia kwa kuvuruga soko la mafuta

Rais Donald Trump wa Marekani sambamba na kuzikosoa Saudi Arabia na Russia kutokana na kuvuruga soko la mafuta, amesema kuwa Riyadh na Moscow zimepatwa na wendawazimu katika suala hilo.

Ameongeza kuwa, vita vya bei ya mafuta kati ya Saudia na Russia vimeisababishia madhara sekta ya mafuta duniani. Mwanzoni mwa mwezi Machi na baada ya upinzani mkali wa serikali ya Russia kuhusu kushushwa zaidi kiwango cha uzalishaji wa nishati hiyo kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona sambamba na kupungua idadi ya waagizaji wake, ulitamatisha makubaliano ya mafuta kati ya Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) na Russia.

Mzozo wa mafuta katika soko la dunia 

Katika upande mwingine ushindani uliopo baina ya Russia na Saudia kama nchi mbili muhimu wazalishaji wa mafuta duniani, umeifanya serikali ya Riyadh kutangaza kiwango chake cha uzalishaji mafuta wa zaidi ya mapipa milioni moja kwa siku. Hii ni katika hali ambayo kutokana na kuenea virusi vya Corona na matokeo yake mabaya, mahitaji ya dhahabu hiyo nyeusi katika soko la dunia yamepungua zaidi. Kwa sasa bei ya mafuta kwenye soko la dunia imeshuka sana kwa kiwango cha chini zaidi ya miaka 18 ya hivi karibuni. Katika miamala ya mwisho katika soko la nishati, bei ya mafuta ghafi ya Texas nchini Marekani ilipungua kwa kiwango cha karibu asilimia 10, kwa dola 19 na senti 35.