Netanyahu afedheheka akitaka kuchafua sura ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60117-netanyahu_afedheheka_akitaka_kuchafua_sura_ya_iran
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu hivi karibuni alionyesha mkanda wa video akidai kuwa unaonyesha jinsi Iran inavyowatupa na kuwazika wahanga wa virusi vya corona jalalani, lakini baadaye kidogo imedhihiri kwamba mkanda huo wa video ni sehemu ya sinema iliyoonyeshwa kwenye televisheni nchini Marekani mwaka 2007.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 02, 2020 03:05 UTC
  • Benjamin Netanyahu
    Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu hivi karibuni alionyesha mkanda wa video akidai kuwa unaonyesha jinsi Iran inavyowatupa na kuwazika wahanga wa virusi vya corona jalalani, lakini baadaye kidogo imedhihiri kwamba mkanda huo wa video ni sehemu ya sinema iliyoonyeshwa kwenye televisheni nchini Marekani mwaka 2007.

Kanali ya 13 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imawanukuu mawaziri wawili wa serikali ya utawala huo wakisema kuwa, baada ya Netanyahu kuonyesha mkanda huo wa video, Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala huo ilitambua kuwa mkanda huo ni sehemu ya filamu fupi iliyoonyeshwa nchini Marekani hapo mwaka 2007. 

Ripoti ya televisheni hiyo ya Israel imeongeza kuwa, Netanyahu alionyesha mkanda huo wa video Jumatatu iliyopita katika kikao cha baraza la mawaziri na kudai kuwa unasimulia jinsi Iran inavyowazika wahanga wa virusi vya corona maeneo ya taka na jalalani. 

Mkanda huo wa video ulianza kuonyeshwa juma lililopita katika kanali za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mitandano ya kijamii na ndipo Benjamin Netanyahu alipouchukua na kuuonyesha kwenye baraza la mawaziri la Israel bila ya kubaini usahihi wake.

Benjamin Netanyahu

Netanyahu na viongozi wa Marekani akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo wamekuwa wakifanya njama za kuchafua jina la Iran na kutilia shaka takwimu rasmi zinazotolewa na Wizara ya Afya ya Iran kuhusu maambukizi na vifo vinavyosababishwa na virusi vya corona.

Hata hivyo katika mahojiano yake ya hivi karibuni na televisheni ya CNN ya Marekani, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Gabrisos alikanusha madai hayo na kusema shirika hilo linasimamia hali katika nchi mbalimbali kwa kutumia vigezo vyake vya kiufundi, na hadi sasa hakuna ushahidi onaoonyesha kwamba, takwimu zinazotolewa na Iran kuhusu maambukizi ya corona si sahihi.