Iran yasema hakuna mazungumzo na Marekani hadi masharti yake yatimizwe
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141472-iran_yasema_hakuna_mazungumzo_na_marekani_hadi_masharti_yake_yatimizwe
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SNSC), Meja Jenerali Mohsen Rezaei, amesisitiza kuwa kauli za mkanganyiko na ujumbe unaotatanisha kutoka kwa Rais wa Marekani haupaswi kumpotosha yeyote kutoka kwenye uhalisia mpya uliopo sasa kuhusu mafuta na milango-bahari, akiongeza kuwa hakutakuwa na mazungumzo yoyote hadi masharti yaliyowekwa na Iran yatimizwe kikamilifu.
(last modified 2026-09-15T04:23:20+00:00 )
Sep 15, 2026 04:18 UTC
  • Meja Jenerali Mohsen Rezaei
    Meja Jenerali Mohsen Rezaei

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (SNSC), Meja Jenerali Mohsen Rezaei, amesisitiza kuwa kauli za mkanganyiko na ujumbe unaotatanisha kutoka kwa Rais wa Marekani haupaswi kumpotosha yeyote kutoka kwenye uhalisia mpya uliopo sasa kuhusu mafuta na milango-bahari, akiongeza kuwa hakutakuwa na mazungumzo yoyote hadi masharti yaliyowekwa na Iran yatimizwe kikamilifu.

Katika ujumbe aliochapisha kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa X usiku wa kuamkia Jumanne, Meja Jenerali Rezaei ameandika hivi: “Msipotoshwe na ishara kinzani za rais wa Marekani kuanzia ‘hakuna mazungumzo’ hadi ‘tuko tayari kuzungumza.’ Mizani ya nguvu na maslahi kuhusu mafuta na milango-bahari imebadilika kabisa. Mbinu za kupunguza athari za hasara (damage control) hazitazuia kile kinachokuja.”

Amesisitiza kuwaL “Hakuna mazungumzo yoyote hadi masharti ya Iran yatimizwe kikamilifu.."

Onyo hili zito limekuja saa chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuchapisha madai kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba “Iran inataka makubaliano kwa haraka na kwa shauku kubwa,” huku akidai kwa jeuri kwamba yeye ndiye “atakayeamua iwapo Marekani itachagua kujihusisha au la,” na kuongeza kuwa “yuko tayari kutafakari kuhusu wazo la mazungumzo.”

Ujumbe huo wa Trump unakinzana waziwazi na msimamo wake wa awali. Mnamo mwezi Agosti, aliwahi kuandika kuwa “hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea, au yaliyopangwa, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” akisisitiza kwamba mzingiro wa baharini bado upo, na akatoa madai ya uongo kwamba Lango-Bahari la Hormuz liko “wazi.” Siku hiyohiyo, mkwe wake ambaye pia ni mjumbe wake, Jared Kushner, alisema kuwa mazungumzo na Iran “huenda ni imara zaidi ya inavyodhaniwa.”

Kadhalika, Trump amekuwa akibadilika-badilika mara kwa mara, kati ya kutoa vitisho vya “kunyakua mafuta ya Iran kama ilivyokuwa Venezuela,” kudai kuwa Iran “inapiga simu mfululizo” kuomba mazungumzo, hadi kudai kuwa vita vitamalizika mara tu baada ya uchaguzi wa kati kati ya muhula nchini Marekani.

Maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametupilia mbali madai hayo na kuyataja kama propaganda tupu na jaribio la kukata tamaa la kufunika kushindwa kwa Washington kulazimisha matakwa yake ya kidhalimu katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Meja Jenerali Rezaei, ambaye pia ni kamanda mkuu wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), amesisitiza kadhaa kwamba njia hiyo nyeti ya kimkakati ya majini inabaki imefungwa na iko chini ya udhibiti kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha amesema wazi kuwa mabadiliko yoyote katika hali hiyo yanategemea hatua thabiti kutoka upande wa Marekani: kukomesha kabisa vita na vikwazo/mzingiro, kuachiliwa huru kwa mali zote za Iran zilizozuiliwa kinyume cha sheria, na kukubali usitishaji vita wa pande zote katika eneo zima la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), ikiwemo kusitisha jinai na uvamizi huko Lebanon na Gaza.