-
Matokeo ya uchaguzi wa bunge wa utawala haramu wa Kizayuni na mpasuko mkubwa wa ndani
Mar 06, 2020 04:07Matokeo ya uchaguzi wa tatu wa bunge la utawala haramu wa Israel katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kabla ya jambo jingine lolote yanaonyesha kuwepo mpasuko mkubwa ndani ya utawala huo.
-
Saudia yapiga marufuku Umrah kutokana na hofu ya kuenea Corona
Mar 05, 2020 07:57Saudi Arabia imewapiga marufuku raia wake na wakazi wa nchi hiyo kutekeleza ibada ya Umrah katika mji wa Makka au kuzuru Msikiti wa Mtume SAW katika mji wa Madina kwa hofu ya kuenea kirusi cha Corona ambacho kinaenea kwa kasi duniani.
-
Wahajiri kutoka Syria, kisingizio kinachotumiwa na Rais Erdoğan wa Uturuki kuushinikiza Umoja wa Ulaya
Mar 05, 2020 03:15Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amelikataa pendekezo la Umoja wa Ulaya kuhusu kadhia ya wahajiri na kusema: Hakuna mtu yeyote mwenye haki na ustahiki wa kuichezea ghururi ya Uturuki. Erdoğan ameyasema hayo mjini Ankara katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya pamoja na Waziri Mkuu wa Bulgaria, Boyko Borisov.
-
Haniya: Shahidi Soleimani alikuwa na nafasi ya "msingi" katika kuiunga mkono Palestina
Mar 05, 2020 00:12Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) aliyeuliwa shahidi alikuwa na nafasi muhimu na ya msingi katika kuunga mkono muqawama.
-
Umuhimu wa hatua ya Ansarullah ya kuukomboa mji wa al Hazm huko Yemen
Mar 04, 2020 22:14Tukiwa mwisho mwa mwaka wa tano tangu Saudi Arabia na washirika wake waanzishe mashambulizi na kuivamia nchi ya Yemen, jeshi la nchi hiyo na makundi ya kujitolea ya wananchi yamefanikiwa kukomboa mji wa al Hazm ambao ni makao makuu ya mkoa wa Al-Jawf.
-
Syria yakaribisha suala la kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu
Mar 04, 2020 09:57Balozi wa Syria nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba serikali ya Damascus inakaribisha kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu, amesema kuwa hata kama baadhi ya tawala za Kiarabu zilihusika kuyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria, lakini raia wa mataifa ya Kiarabu wameonyesha huruma kwa raia wa Syria.
-
Askari wa Uturuki wakimbia kwa makundi katika viunga vya Idlib, Syria + Video
Mar 04, 2020 09:54Kufuatia mashambulizi makali ya anga na mizinga ya jeshi la Syria dhidi ya maeneo ya jeshi la Uturuki katika viunga vya mkoa wa Idlib, askari wa Uturuki wameonekana wakikimbia kwa makundi katika maeneo hayo.
-
Thabo Mbeki: Tutalinda mirathi ya Mandela ya kuliunga mkono taifa la Palestina
Mar 04, 2020 08:31Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki ameonyesha wasiwasi wake wa kupungua himaya na uungaji mkono kwa Palestina na kueleza kwamba, nchi yake itaendelea kulinda mirathi ya hayati Nelson Mandela pamoja na miongozo yake ya kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina.
-
Makundi ya muqawama Palestina yasisitiza kupambana na siasa haribifu za Marekani
Mar 04, 2020 08:24Makundi ya Muqawama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu yamesisitiza juu ya kukabiliana na siasa haribifu za Marekani dhidi ya wananchi wa Palestina pamoja na njama za Kizayuni-Kimarekani kupitia mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne.
-
Corona yawaweka chini ya karantini makumi ya watu nchini Saudi Arabia
Mar 04, 2020 04:01Watu wasiopungua 70 wamewekewa chini ya karantini na uangalizi maalumu wa madaktari huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mtu aliyethibitika kukumbwa na ugonjwa huo nchini humo.