Syria yakaribisha suala la kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59548-syria_yakaribisha_suala_la_kupanuliwa_uhusiano_na_nchi_za_kiarabu
Balozi wa Syria nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba serikali ya Damascus inakaribisha kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu, amesema kuwa hata kama baadhi ya tawala za Kiarabu zilihusika kuyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria, lakini raia wa mataifa ya Kiarabu wameonyesha huruma kwa raia wa Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 04, 2020 09:57 UTC
  • Syria yakaribisha suala la kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu

Balozi wa Syria nchini Lebanon sambamba na kubainisha kwamba serikali ya Damascus inakaribisha kupanuliwa uhusiano na nchi za Kiarabu, amesema kuwa hata kama baadhi ya tawala za Kiarabu zilihusika kuyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini Syria, lakini raia wa mataifa ya Kiarabu wameonyesha huruma kwa raia wa Syria.

Sambamba na kubainisha kwamba hivi sasa serikali ya Damascus inafuatilia suala la kukomboa kikamilifu ardhi zake zinazodhibitiwa na magaidi, Ali Abdul Karim, balozi wa Syria nchini Lebanon ameongeza kuwa ugaidi ni tishio kwa Syria na Lebanon na suala hilo linabainisha udharura wa kuwepo ushirikiano kati ya Beirut na Damascus katika nyuga za kiuchumi, kisiasa na kiusalama. Kadhalika Ali Abdul Karim ameashiria mshikamano uliopo kati ya jeshi la Syria na Lebanon katika mapambano yao dhidi ya ugaidi na kubainisha kwamba, uhusiano na mshikamano wa kiusalama kati ya nchi mbili, unazingatia maslahi ya kiusalama.

Baadhi ya nchi za Kiarabu kama vile Saudia, ndio waungaji mkono wakubwa wa makundi ya kigaidi

Balozi wa Syria nchini Lebanon sambamba na kusisitiza kwamba taifa la Lebannon ni lazima lijifakharishe kwa mafanikio ya muqawama ndani ya nchi hiyo, amesisitiza kuwa baada ya muqawama wa Lebanon kupata ushindi katika kukabiliana na uvamizi wa Wazayuni mwaka 2000, na licha ya baadhi ya njama za kimataifa na kieneo, ulipata ushindi mwingine mwaka 2006.