Makundi ya muqawama Palestina yasisitiza kupambana na siasa haribifu za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59540-makundi_ya_muqawama_palestina_yasisitiza_kupambana_na_siasa_haribifu_za_marekani
Makundi ya Muqawama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu yamesisitiza juu ya kukabiliana na siasa haribifu za Marekani dhidi ya wananchi wa Palestina pamoja na njama za Kizayuni-Kimarekani kupitia mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Mar 04, 2020 08:24 UTC
  • Makundi ya muqawama Palestina yasisitiza kupambana na siasa haribifu za Marekani

Makundi ya Muqawama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu yamesisitiza juu ya kukabiliana na siasa haribifu za Marekani dhidi ya wananchi wa Palestina pamoja na njama za Kizayuni-Kimarekani kupitia mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne.

Khalid al-Batsh, mmoja wa wajumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad al-Islami Palestina ameashiria katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya al-Mayadeen juu ya umoja wa makundi ya Palestina kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisiasa na kusema kuwa, kuna ulazima wa kukabiliana na siasa haribifu na zilizojaa njama za serikali ya Washington katika eneo hili.

Aidha amesema kuwa, Harakati ya Jihad al-Islami inapinga kuweko uhusiano wa aina yoyote ile na serikali ya Marekani.

Khalid al-Batsh amesema kuwa, nchi za Kiarabu zinazofuatiliana suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kimsingi zinataka kutekeleza mipango ya Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi.

Khalid al-Batsh, mmoja wa wajumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad al-Islami Palestina

Kwa upande wake Sabri Saidam, mmoja wa wajumbe waandamizi wa Harakati ya Fat’hi amesema kuwa, serikali ya Marekani inatafuta washirika huko Palestina kwa ajili ya kutekeleza mpango wa Muamala wa karne. Amesisitiza kuwa, kuendelea hitilafu baina ya makundi ya Kipalestina kutakuwa ni kuunga mkono mpango wa Marekani na Wazayuni wa Muamala wa Karne.

Kwa mujibu wa mpango huo, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na makundi ya muqawama hayataruhusiwa kumiliki silaha.