-
Serikali ya Syria: Hatutaki uvamizi wa aina yoyote ile katika ardhi yetu
Feb 05, 2020 01:13Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, amesema kuwa raia wa nchi hiyo hawakubali uvamizi wowote katika ardhi za nchi yao.
-
Denmark na Uholanzi zawaita mabalozi wa Saudia kulalamikia ujasusi
Feb 04, 2020 21:43Serikali za Denmark na Uholanzi zimewaita mabalozi wa Saudi Arabia katika miji ya Copenhagen na Stockholm, kuwasilisha malalamiko rasmi baada ya nchi mbili hizo za Ulaya kuwatia mbaroni magaidi wanne waliokuwa wakifanya ujasusi kwa niaba ya Riyadh.
-
Muungano wa 'Sairoon' kuchunguza mpango wa kuwatimua haraka askari wa Kimarekani nchini Iraq
Feb 04, 2020 10:42Muungano wa 'Sairoon' katika bunge la Iraq umeitisha kikao kikuu cha kitaifa kwa ajili ya kuchunguza mpango wa kuwatimua haraka askari wa Marekani kutoka katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Mapigano yashtadi kati ya majeshi ya Uturuki na Syria, askari kadhaa wa pande mbili wauawa
Feb 04, 2020 04:10Askari kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mapigano kati ya majeshi ya Syria na Uturuki yaliyotokea kwenye eneo la kaskazini ya ardhi ya Syria.
-
Russia yatiwa wasi wasi na mashambulizi ya magaidi katika mkoa wa Idlib, Syria
Feb 04, 2020 01:15Serikali ya Russia imetoa radiamali yake kufuatia baadhi ya ripoti zinazohusu kushambuliwa askari wa Uturuki katika operesheni zinazofanywa na askari wa Syria.
-
Usama Hamdan: Muamala wa Karne ni sehemu ya njama za Marekani za kuiangamiza Palestina
Feb 03, 2020 23:11Mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesisitiza kuwa, mpango wa Muamala wa Karne ni sehemu ya njama za Marekani zenye lengo la kuiangamiza kadhia ya Palestina na kuhalalisha uwepo wa utawala vamizi wa Israel katika Asia Magharibi.
-
Askari 15 wa Kizayuni wajeruhiwa vibaya wakati wakifanya majaribio ya silaha
Feb 03, 2020 23:09Vyombo vya habari vimeripoti kwamba kwa akali askari 15 wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamejeruhiwa vibaya wakati wakifanya majaribio ya silaha.
-
Pakistan: Matumaini ya Trump kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Kashmir, ni ujinga mkubwa
Feb 03, 2020 12:24Seneta wa ngazi ya juu nchini Pakistan sambamba na kubainisha kwamba Marekani kamwe haijawahi kuwatakia jambo la kheri Waislamu, amesema kuwa Trump hataki hata kidogo kutatuliwa matatizo ya Waislamu wa Kashmir.
-
Wapalestina wataka OIC ilaani mpango wa Muamala wa Karne; Saudia na Imarati zakataa
Feb 03, 2020 08:58Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wamekutana leo katika mkutano wao wa dharura mjini Jeddah, Saudi Arabia kwa minajili ya kujadili mpango uliopendekezwa na Marekani ambao unakandamiza haki za taifa la Palestina.
-
"Muamala wa Karne"; njama itakayotupiliwa mbali kwenye jalala la taka la historia
Feb 03, 2020 04:11Rais Donald Trump wa Marekani wiki iliyopita alizindua mpango mpya kwa jina la "Muamala wa Karne" kwa madai ya kuhitimisha mzozo baina ya Palestina na utawala ghasibu wa Israel. Mpango ambao kama wanavyoamini aghalabu ya weledi wa mambo utagonga mwamba tu kama ilivyokuwa mipango mingine ya huko nyuma kutokana na sababu zilizo wazi.