Askari 15 wa Kizayuni wajeruhiwa vibaya wakati wakifanya majaribio ya silaha
(last modified Tue, 04 Feb 2020 02:39:23 GMT )
Feb 04, 2020 02:39 UTC
  • Askari 15 wa Kizayuni wajeruhiwa vibaya wakati wakifanya majaribio ya silaha

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba kwa akali askari 15 wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamejeruhiwa vibaya wakati wakifanya majaribio ya silaha.

Kwa mujibu wa habari hiyo, askari hao wameripukiwa na kombora katika moja ya majaribio ya silaha waliyokuwa wakiyafanya katika maeneo ya kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (yaani Israel) ambapo kwa akali askari 15 wa kikosi cha Golan wamejeruhiwa vibaya. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa utawala huo katili wanawatambua askari wa kikosi cha Golan kuwa wenye nguvu kubwa zaidi katika jeshi la utawala huo haramu. Aidha Jumapili jeshi la utawala huo lilifanya maneva ya kijeshi kwa kuunda mfano wa vita katika pande kadhaa ambapo askari wa nchi kavu, majini, anga na kadhalika wa upelelezi wa Israel walishiriki maneva hayo.

Muqama ambao umeitia kiwewe Israel

Katika hotuba zao za hivi karibuni viongozi wa Israel walitabiri kwamba baada ya kuzinduliwa mpango wa Muamala wa Karne, utawala huo khabithi utakumbwa na tishio kutoka pande kadhaa ikiwemo Lebanon, Syria na Ukanda wa Gaza. Rais Donald Trump wa Marekani pamoja na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel walizindua mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne Jumanne iliyopita, mpango ambao umeendelea kupingwa kote duniani.

Tags