Denmark na Uholanzi zawaita mabalozi wa Saudia kulalamikia ujasusi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58947-denmark_na_uholanzi_zawaita_mabalozi_wa_saudia_kulalamikia_ujasusi
Serikali za Denmark na Uholanzi zimewaita mabalozi wa Saudi Arabia katika miji ya Copenhagen na Stockholm, kuwasilisha malalamiko rasmi baada ya nchi mbili hizo za Ulaya kuwatia mbaroni magaidi wanne waliokuwa wakifanya ujasusi kwa niaba ya Riyadh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2020 21:43 UTC
  • Denmark na Uholanzi zawaita mabalozi wa Saudia kulalamikia ujasusi

Serikali za Denmark na Uholanzi zimewaita mabalozi wa Saudi Arabia katika miji ya Copenhagen na Stockholm, kuwasilisha malalamiko rasmi baada ya nchi mbili hizo za Ulaya kuwatia mbaroni magaidi wanne waliokuwa wakifanya ujasusi kwa niaba ya Riyadh.

Idara ya Usalama na Intelijensia ya Denmark imetangaza habari ya kuwatia mbaroni wanachama watatu wa kundi la kigaidi la al-Ahvaziya linaloipiga vita serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo wameshitakiwa kwa kufanya vitendo vya kijasusi kwa niaba ya Riyadh ndani ya nchi hiyo ya Ulaya.

Gaidi mwingine amekamatwa nchini Uholanzi kwa kufanya ujasusi pia kwa niaba ya utawala wa Riyadh.

Finn Borch Andersen, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Intelijensia ya Denmark amewaambia waandishi wa habari mjini Copenhagen kuwa, wanachama hao wa Vuguvugu la Kiarabu la Kutaka Kukombolewa Ahvaz (al-Ahvaziya) wanaandamwa na mashitaka ya kufanya vitendo vya kijasusi kwa niaba ya Saudia nchini humo, kati ya mwaka 2012 na 2018.

Bendera za Saudia, Denmark na Uholanzi

Polisi ya Denmark inawatuhumu magaidi hao watatu kwa kuunga mkono shambulizi la kigaidi dhidi ya Iran mnamo Septemba mwaka 2018, ambapo watu 25 akiwemo mtoto mdogo wa miaka minne waliuawa.

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Steve Block amethibitisha habari ya kuitwa balozi wa Saudia nchini humo na kukabidhiwa malalamiko rasmi ya kutiwa mbaroni gaidi na jasusi wa Saudia nchini humo.