-
Japan yafunga kinu cha nyuklia cha Fukushima baada ya tetemeko la ardhi nchini Russia
Jul 30, 2025 09:14Japan leo Jumatano imewahamisha wafanyakazi wote wa kinu cha nyuklia cha Fukushima mashariki mwa nchi hiyo ikihofia athari za tetemeko kubwa la ardhi lililopiga pwani ya Rasi ya Kamchatka mashariki mwa Russia mapema leo asubuhi.
-
Wagiriki wawazuia watalii wa Israel kuingia katika fukwe za Ugiriki
Jul 30, 2025 04:17Kufuatia mauaji ya watu wa Gaza na kuzuiwa misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo; wananchi wa Ugiriki hawawaruhusu tene watalii wa Israel kuingia katika visiwa vya nchi yao, suala ambalo limesababisha mapigano kati yao na polisi wa Ugiriki.
-
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.7 laikumba pwani ya Russia, tahadhari ya Tsunami yatolewa
Jul 29, 2025 23:41Tahadhari za kuzuka Tsunami zimetolewa katika nchi kadhaa baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.7 kulikumba eneo la mashariki ya Russia la Peninsula ya Kamchatka.
-
Uholanzi yawazuia kuingia nchini Ben-Gvir na Smotrich kwa kuchochea machafuko na maangamizi ya kizazi Ghaza
Jul 29, 2025 23:24Uholanzi imewataja mawaziri wa Israeli Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich kuwa watu wasiokubalika na hivyo imewapiga marufuku kuingia nchini humo kutokana na vitendo vyao vya kuwachochea walowezi wa Kizayuni kuendesha ghasia na vitendo vya mabavu dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na maangamizi ya kizazi katika Ukanda wa Gaza.
-
Je, ni hatua gani ya hivi majuzi ya rais wa Colombia dhidi ya Israel?
Jul 29, 2025 23:11Rais wa Colombia Gustavo Petro hivi karibuni alitoa amri ya kuzuia mauzo ya makaa ya mawe ya nchi hiyo kwa utawala wa Israel.
-
Gaidi jijini New York auwa watu 4, wakiwemo afisa wa polisi Mwislamu
Jul 29, 2025 07:54Gaidi alieykuwa na silaha alifyatua risasi ndani ya jengo refu la kifahari jijini Manhattan, New York, na kuua watu wanne, akiwemo afisa wa polisi Mwislamu mwenye asili ya Bangladesh kabla ya kujitoa uhai.
-
Katibu Mkuu wa UN: Suluhisho la mataifa mawili liko hatarini, zinatakiwa hatua za haraka
Jul 29, 2025 03:30Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa indhari kali akisema, suluhisho la mataifa mawili ya Palestina na Israel “liko mbali zaidi sasa hivi kuliko wakati wowote” na kwamba dunia imefikia “kiwango cha kukata tamaa” ya kufanikisha lengo hilo.
-
Korea Kaskazini: Lazima US ikubali sisi ni dola la nyuklia, kutupokonya silaha ni 'dhihaka'
Jul 29, 2025 03:29Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameitaka Marekani ikubali hali "isiyoweza kutenduliwa" ya nchi hiyo kuwa taifa linalomiliki silaha za nyuklia, na kuonya kwamba mazungumzo hayataweza kamwe kupelekea kufutwa uwezo wake wa nyuklia.
-
Katibu Mkuu wa UN ataka jamii ya kimataifa ipinge matumizi ya njaa kama silaha ya vita
Jul 28, 2025 23:17Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa ipinge matumizi ya njaa kama silaha ya vita.
-
Mmarekani aliyemuua mtoto wa Kipalestina afariki dunia gerezani
Jul 28, 2025 23:11Mwenye nyumba huko Illinois aliyepatikana na hatia ya kumuua mtoto wa mpangaji wake Mmarekani mwenye asili ya Palestina amefariki dunia akiwa kizuizini.