Wagiriki wawazuia watalii wa Israel kuingia katika fukwe za Ugiriki
Kufuatia mauaji ya watu wa Gaza na kuzuiwa misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo; wananchi wa Ugiriki hawawaruhusu tene watalii wa Israel kuingia katika visiwa vya nchi yao, suala ambalo limesababisha mapigano kati yao na polisi wa Ugiriki.
Televisheni ya al Masira ya Yemen imevinukuu vyombo vya habari vya Ugiriki na kuripoti kuwa: Katika kisiwa cha Krete, kumejiri mapigano kati ya polisi na waandamanaji wa Kigiriki wanaopinga kuwasili kwa meli ya starehe ya Israel.
Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, maandamano na upinzani wa wananchi wa Ugiriki dhidi ya kuwasili katika fukwe za nchi hiyo watalii wa Kizayuni ni tukio la tatu kushuhudiwa katika viswa vya Ugiriki hivi karibuni.
Wakati huo huo jarida la Politico linalochapishwa Marekani limeripoti kuwa, upinzani na maandamano yameshika kasi nchini Ugiriki kutokana na kushtadi kwa mashambulizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Gaza.