-
Waliofariki dunia klabuni Jamhuri ya Dominika wafikia 218
Apr 10, 2025 22:33Maafisa wa serikali katika Jamhuri ya Dominika wamesema idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mkasa wa kuporomoka kwa paa katika ukumbi wa starehe wa Jet Set katika mji mkuu Santo Domingo imepindukia 200, huku matumaini ya kupata manusura yazidi kukififia.
-
Ripoti: Putin analenga 'adui mpya wa Kimagharibi': Waabudu Shetani
Apr 10, 2025 08:42Rais wa Russia, Vladimir Putin na washirika wake wamevitaja vita vya Ukraine kuwa vita dhidi ya waabudu mashetani, na vilevile dhidi ya sera zinazounga mkono vitendo vya maingiliano ya kingono baina ya watu wenye jinsia moja (LGBTQ) za Magharibi, ambazo wanaona kuwa zinadhoofisha maadili ya jadi ya Kikristo.
-
Viongozi wa Amerika ya Latini watoa wito kupinga ushuru wa Trump
Apr 10, 2025 08:02Viongozi wa nchi za Amerika ya Latini wametaka kuweko umoja na mshikamano wa kukabiliana na ushuru wa Rais Donald Trump wa Marekani na kuyumba uchumi kunakosababishwa na hatua hizo za Trump.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza: Trump anaiburuta dunia katika ukingo wa mdodoro wa uchumi
Apr 10, 2025 07:53Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ametahadharisha kuwa sera za kibiashara za Rais Donald Trump wa Marekani zinauelekeza uchumi wa dunia katika mdodoro hatari wa kiuchumi; na ni kupitia tu kuratibiwa hatua za kimataifa ndipo tunaweza kuzuia kukaririwa mgogoro wa uchumi kama ule ulioiathiri dunia mwaka 2008.
-
Sera za ushuru za Trump na ukuruba wa China na Ulaya
Apr 10, 2025 07:14Sera za ushuru za Rais Donald Trump wa Marekani zimegeuka kuwa vita vya kibiashara kati ya Marekani na waitifaki, washirika na wapinzani wake wa kibiashara.
-
Russia: Dunia imechoshwa na vitisho visivyokwisha vya Marekani dhidi ya Iran
Apr 10, 2025 04:17Russia imelaani vikali vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema dunia imechoshwa na hali hiyo.
-
China yajibu mapigo; yaongeza ushuru wa 84% kwa bidhaa za US
Apr 09, 2025 23:24China imesisitiza kuwa "itapambana hadi mwisho" mkabala wa vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Ubelgiji nayo yatia ulimi puani, yasema: Hatutamkamata Netanyahu
Apr 09, 2025 03:05Ubelgiji nayo pia imetangaza kuwa haitotii amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya kutaka waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe na kukabidhiwa kwa mahakama hiyo.
-
Kamanda Mkuu wa US Ulaya: Mauzo ya silaha za Marekani kwa Ulaya yameongezeka kwa 600%
Apr 09, 2025 03:04Kamanda Mkuu wa Marekani katika Kamandi ya jeshi la nchi hiyo barani Ulaya amesema, mauzo ya silaha za Marekani kwa nchi za Ulaya yameongezeka kwa asilimia 600 tangu vilipoanza vita kati ya Russia na Ukraine na akaongeza kuwa, thamani ya kiwango cha silaha zilizoagizwa na nchi za Ulaya tangu vilipoanza vita kati ya Russia na Ukraine hadi sasa imefikia dola bilioni 265.
-
Netanyahu apigwa na butwaa mbele ya kamera baada ya Trump kutangaza mazungumzo na Iran
Apr 08, 2025 23:11Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, alionekana kukumbwa na mshtuko na mshangao wa ghafla katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Marekani, Donald Trump, baada ya Trump kutangaza kwamba mazungumzo kati ya Washington na Tehran yataanza Jumamosi.