-
Waziri Mkuu mteule asema Greenland katu haitauzwa, aitaka Ulaya isimame nayo kukabiliana na Trump
Mar 16, 2025 07:20Waziri Mkuu mteule wa Greenland Jens-Frederik Nielsen ameziomba nchi za Ulaya zisimame pamoja nayo na kusisitiza kuwa eneo hilo si la kuuzwa.
-
Hatua ya Marekani ya kuishambulia kijeshi Yemen; kukariri mkakati ulioshindwa kufua dafu mbele ya Ansarullah
Mar 16, 2025 06:14Donald Trump, ambaye aliingia madarakani kwa ahadi ya kuleta suluhu na amani na kuhitimisha vita kadhaa wa kadhaa vilivyoanzishwa na Marekani, ametoa amri ya kushambuliwa kijeshi Yemen baada ya kupita miezi miwili tu tangu ashike hatamu za utawala.
-
Canada kuangalia upya mkataba wa kununua ndege za kivita za Marekani
Mar 16, 2025 02:34Waziri Mkuu mpya wa Canada, Mark Carney ametoa amri ya kupitiwa upya mkataba wa nchi hiyo na kampuni ya silaha ya Marekani unaohusiana na kuiuzia Canada ndege za kivita za F-35.
-
Wasiwasi wa afisa wa ngazi ya juu wa Marekani kuhusu kufichuliwa taarifa za siri za nchi hiyo
Mar 15, 2025 23:18Mkurugenzi wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani, Tulsi Gabbard, amesema wale wote waliofichua taarifa za siri watakabiliwa na hatua kali na kwamba suala hili haliwezi kuvumiliwa.
-
Mgongano wa maneno na vitendo vya seriakli ya Trump kuhusu Iran
Mar 15, 2025 22:48Licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kuzungumzia mara kwa mara nia yake ya kufanya mazungumzo na Iran katika miezi ya kwanza ya muhula wake wa pili wa urais na hata kutuma barua kuhusiana na suala hilo kwa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, lakini kivitendo amekuwa akitekeleza mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran na kuchukua hatua mpya katika uwanja huo kila siku.
-
UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'
Mar 15, 2025 11:07Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya "ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu", akitoa wito kwa serikali kulinda uhuru wa kidini, na kwa majukwaa ya mtandaoni kuzuia matamshi ya chuki.
-
Utawala wa Trump kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43
Mar 15, 2025 09:36Gazeti la New York Times limeandika katika toleo lake la leo kuwa serikali ya Donald Trump inapitia mpango wa kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43.
-
Mtikisiko wa kiuchumi nchini Uingereza; Kengele ya hatari kwa serikali ya Starmer
Mar 15, 2025 05:12Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa uchumi wa Uingereza ulidorora mwanzoni mwa 2025, kinyume na utabiri, na kushuka huku kusikotarajiwa, ambako ni matokeo ya uzalishaji duni wa viwandani na kudorora kwa sekta muhimu, kumezidisha wasiwasi kuhusu mustakabali wa uchumi wa nchi hiyo na changamoto zinazoikabili serikali ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer katika njia ya ukuaji wa uchumi.
-
Marekani yamfukuza Balozi wa Afrika Kusini kwa 'kujieleza'
Mar 15, 2025 03:41Msuguano baina ya Marekani na Afrika Kusini umeendelea kutokota, baada ya Washington kumtangaza Balozi wa nchi hiyo ya Kiafrika mjini Washington, Ebrahim Rasool, kuwa mtu asiyetakiwa, kufuatia matamshi yake ya kumkosoa Rais Donald Trump.
-
Maafisa wa US yumkini wakapelekwa ICC kwa kuzuia haki
Mar 15, 2025 03:40Afisa wa zamani wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Craig Mokhiber ameonya kuwa, maafisa wa Marekani wanaoishambulia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC katika kuitetea Israel wanazuia haki na sheria, na kusisitiza kwamba wanaweza kushtakiwa katika siku zijazo.