-
Russia yaahidi kufanya mashambulio zaidi baada ya kuishambulia gridi ya umeme ya Ukraine
Nov 28, 2024 23:01Zaidi ya watu milioni moja nchini Ukraine wameachwa gizani baada ya Russia kushambulia maeneo mbalimbali ya kijeshi ya nchi hiyo pamoja na gridi ya umeme.
-
Biden akaidi amri ya mahakama ya ICC, aidhinisha kuipatia silaha zaidi Israel
Nov 28, 2024 07:55Rais Joe Biden wa Marekani amepuuza hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya kukamatwa viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutenda jinai za kivita, kwa kupasisha kutuma silaha za mamia ya mamilioni ya dola kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wabunge wa Marekani wawasilisha muswada wa kuadhibu vyuo vikuu vinavyoitenga na Israel
Nov 28, 2024 07:54Wabunge wawili wa Marekani wamewasilisha muswada wenye utata ambao utazuia ufadhili wa Serikali ya Shirikisho kwa vyuo vikuu vinavyoshiriki katika kampeni ya "susia Israel kibiashara", baada ya mwaka mmoja wa uhamasishaji mkubwa wa kuwatetea Wapalestina katika vyuo vikuu nchini Marekani mkabala wa vita vya mauaji ya kimbari ya utawala haramu wa Israel.
-
Mbunge Uhispania ashiriki mgomo wa kula kuunga mkono Palestina
Nov 27, 2024 23:26Mbunge mmoja nchini Uhispania, Jorge Pueyo, ametangaza kushiriki katika mgomo wa kula chakula ikiwa ni njia ya kuunga mkono wananchi wa Palestina waliozingirwa na kunyimwa chakula huko Gaza.
-
Sisitizo la Trump la kuanza duru mpya ya vita vya ushuru katika kipindi cha pili cha urais
Nov 27, 2024 23:21Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa katika siku yake ya kwanza akiwa Ikulu ya White House, atatoa agizo la kutozwa ushuru mpya bidhaa zote zinazoagizwa kutoka Mexico, Canada na China.
-
Rais wa Russia asisitiza kuanzishwa mfumo wa dunia wa kambi kadhaa na wa haki zaidi
Nov 27, 2024 09:00Rais Vladimir Putin wa Russia amezungumza sambamba na kuwadia safari yake ya kuitembelea Kazakhstan na kusisitiza kuwa, nchi hizo mbili ziko mstari wa mbele katika mchakato wa kuunda mfumo wa dunia wa kambi kadhaa na wenye haki zaidi na pande hizo mbili zina misimamo inayofanana kuhusu mahusiano ya kimataifa na masuala ya usalama wa dunia.
-
Spika wa Uturuki: Kwa maamuzi ya Mahakama mbili za Kimataifa, Israel inaona mwisho wake unakaribia
Nov 27, 2024 08:36Spika wa Bunge la Uturuki Numan Kurtulmus amesema, hati ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya kukamatwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa ulinzi wa utawala huo Yoav Gallant ni kielelezo cha hatua nyingine kubwa inayoonyesha kuwa Israel sasa "inagusika".
-
Human Rights Watch yataka uungaji mkono wa Ulaya kwa waranti ya kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni
Nov 27, 2024 04:14Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesisitiza na kutaka kuwepo uungaji mkono wa Umoja wa Ulaya kwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wa kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kutokana na kuhusika kwake katika jinai za kivita.
-
Maandamano makubwa yafanyika Uhispania kulaani jinai za utawala wa Kizayuni
Nov 27, 2024 02:52Maandamano yamefanyika katika miji tofauti ya Uhispania kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Borrell ataka kutekelezwa uamuzi wa mahakama ya ICC dhidi ya Netanyahu na Gallant
Nov 26, 2024 23:47Kamishna wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, ametoa wito wa kutekelezwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na waziri wake wa zamani wa vita, Yoav Galant.