-
Putin: Tuko tayari kusimamisha vita nchini Ukraine
Nov 16, 2024 03:54Ikulu ya Russia imetangaza habari ya kufanyika mazungumzo ya simu baina ya Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz ambapo Putin amesema kuwa nchi yake iko tayari kuanzisha mazungumzo ya kusimamisha vita nchini Ukraine.
-
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Belfast wamfukuza Clinton, wasema anatetea mauaji ya kimbari Gaza
Nov 15, 2024 08:38Polisi wa Ireland Kaskazini wamemuokoa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hilary Clinton kwa kumuondoa kwenye Chuo Kikuu cha Malkia huko Belfast ambapo mamia ya wanafunzi walikusanyika kulaani msimamo wake kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Gaza.
-
Mashabiki wazomea wimbo wa taifa wa Israel katika mechi ya soka nchini Ufaransa
Nov 15, 2024 07:46Mashabiki wa soka waliohudhuria mechi ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya mjini Paris kati ya Ufaransa na utawala wa Kizayuni wa Israel walipiga filimbi na kuzomea wakati wimbo wa taifa wa utawala huo ulipopigwa mwanzoni mwa mchezo huo.
-
WHO: Wagonjwa wa surua wameongezeka duniani
Nov 15, 2024 04:16Shirika la Afya Duniani (WHO) na lile la Marekani CDC yametangaza kuwa, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa surua kiliongezeka duniani kwa asilimia 20 kati ya mwaka 2022 na 2023.
-
Russia yaitahadharisha Ufaransa kuhusu kutuma makombora Ukraine
Nov 15, 2024 00:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametahadharisha kuhusu Ufaransa kutuma makombora nchini Ukraine.
-
Utafiti: Idadi ya wagonjwa wa kisukari duniani imeongezeka
Nov 14, 2024 07:42Utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa, idadi ya watu wazima wanaougua kisukari duniani kote imeongezeka maradufu katika miongo mitatu iliyopita, huku ongezeko kubwa likishuhudiwa katika nchi zinazoendelea.
-
Ripoti: Ujerumani inaajiri wakimbizi wakapigane vita kama mamluki wa Israel
Nov 14, 2024 03:23Mashirika ya intelijensia ya Ujerumani na ya Kizayuni kwa uratibu wa karibu na utawala wa Tel Aviv yameripotiwa kwamba, yamekuwa yakiwaajiri wakimbizi kutoka nchi zilizokumbwa na vita ili wawe mamluki wa kutumiwa vitani na Israel katika vita dhidi ya Ghaza na Lebanon.
-
Mbunge wa UK: FIFA na UEFA zina 'nyuso mbili za ubaguzi wa rangi' kwa maslahi ya Israel
Nov 14, 2024 02:38Mbunge wa chama cha Leba nchini Uingereza Zarah Sultana amekosoa vikali mashirikisho ya juu ya soka duniani ya FIFA na UEFA kwa kutoziadhibu timu za soka za Israel wakati utawala huo wa Kizayuni unaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Gazeti maarufu la Guardian lajiondoa kwenye X kulalamikia hisia hasi na mielekeo ya ubaguzi
Nov 14, 2024 02:28Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limetangaza kuwa litaacha kuweka maandiko yake kwenye X, mtandao wa kijamii uliokuwa ukijulikana kama Twitter.
-
Waislamu wana wasiwasi kuhusu ongezeko la ubaguzi katika nchi za Ulaya
Nov 13, 2024 23:13Shirika la Haki za Msingi la Umoja wa Ulaya limetangaza kwamba Waislamu wa bara hilo wameathiriwa na ongezeko kubwa la ubaguzi wa rangi na wana wasiwasi mkubwa.