-
Afrika Kusini yatoa ushahidi ICJ kuonesha Israel inavyowatesa kwa njaa Wapalestina wa Ghaza
Nov 13, 2024 08:29Afrika Kusini imesema, ushahidi iliotoa katika kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) unaonyesha jinsi Tel Aviv inavyotumia njaa kama silaha ya vita, lengo likiwa ni kuifanya Ghaza isibaki kuwa na wakazi Wapalestina kwa kuwamaliza kupitia mbinu ya mauaji ya kimbari na kuwahamisha kwa nguvu.
-
Imani ya dini ya vijana Wakristo Ujerumani inapungua kulinganisha na ya vijana wa Kiislamu
Nov 13, 2024 08:23Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa na taasisi ya Ujerumani ya Shell Jugendstudie (Shell Youth Study) yanaonyesha kuwa, nafasi ya imani ya dini katika maisha ya vijana wa Kikristo nchini humo imepungua kwa kiasi kikubwa; na kinyume chake, utafiti huo unaonyesha kuwa, imani juu ya dini miongoni mwa vijana Waislamu ingali ni madhubuti na yenye umuhimu katika maisha yao ya kila siku.
-
Wamarekani Waarabu waliompigia kura Trump wamhimiza asimamishe vita Ghaza na Lebanon
Nov 13, 2024 08:17Wamarekani Waarabu waliompigia kura Donald Trump katika mji wenye Waislamu wengi wa Dearborn, jimboni Michigan wamemtaka rais huyo mteule atoe mwito wa kusitishwa vita mara moja huko Palestina na Lebanon.
-
Iran, Russia na Uturuki zalaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina
Nov 12, 2024 22:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na Uturuki zimetoa taarifa ya pamoja zikilaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi ya utawala huo ghasibu dhidi ya Lebanon na Syria.
-
Miito ya kutimuliwa uwanachana Israel Umoja wa Mataifa yazidi kuongezeka
Nov 12, 2024 22:50Mataifa mbalimbali duniani yameendelea kutoa wito wa kufutiwa uanachama Israel katika Umoja wa Mataifa kutokana na jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina na Lebanon.
-
Matukio ya Amsterdam dhihirisho la utambulisho halisi wa Wazayuni
Nov 12, 2024 22:45Kinyume na riwaya na simulizi iliyogeuzwa ya ghasia za Wazayuni huko Amsterdam Uholanzi, sasa Wazayuni wavamizi katika nchi nyingine za Ulaya pia wanahisi kutokuwa na usalama.
-
Mkutano wa UN kuhusu hali ya hewa waanza Baku, viongozi nchi kubwa wahepa
Nov 12, 2024 09:29Mkutano wa Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa (COP29) unendelea huko Baku nchini Azarbaijan, huku baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa duniani wakikwepa kuhudhuria, wakiwemo viongozi wa China, Marekani, India, Ujerumani na Ufaransa.
-
Wanafunzi wa Kiyahudi waandamana London kumuunga mkono Ripota wa Umoja wa Mataifa, Albanese
Nov 12, 2024 09:15Wanafunzi wa Kiyahudi wamefanya maandamano mbele ya Shule ya Mafunzo ya Mashariki na Afrika katika Chuo Kikuu cha London wakitangaza uungaji mkono wao kwa Ripota wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika maeneo ya Palestina, Francesca Albanese.
-
Trump amteua Mrepublican mkereketwa wa Israel na adui mkubwa wa Iran kuwa balozi UN
Nov 12, 2024 09:15Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mbunge wa chama cha Republican Elise Stefanik, muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel na mpinzani mkali wa Iran kuwa balozi ajaye katika Umoja wa Mataifa.
-
Ufaransa yapiga marufuku bendera ya Palestina katika mechi ya soka kati ya nchi hiyo na Israel
Nov 12, 2024 03:39Mamlaka za Ufaransa zimetumia kisingizio cha fujo zilizotokea wiki iliyopita nchini Uholanzi, kupiga marufuku watazamaji kubeba bendera ya Palestina kwenye mechi ya soka baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel itakayochezwa siku ya Alkhamisi katika kitongoji cha Paris.