-
Kiongozi Mkuu wa Kanisa UK ashinikizwa ajiuzulu kwa kunyamazia udhalilishaji wa kingono
Nov 12, 2024 03:38Mkuu wa Kanisa la Uingereza, ambaye ni kiongozi wa kiroho wa Kanisa la Kianglikana duniani anashinikizwa ajiuzulu baada ya uchunguzi kubaini kuwa alishindwa kuwajulisha polisi mara tu alipofahamu kuhusu unyanyasaji wa kimwili na udhalilishaji wa kingono uliofanywa na mfanyakazi wa kujitolea katika kambi za Kikristo za msimu wa joto.
-
Kushadidi hitilafu katika Umoja wa Ulaya
Nov 12, 2024 00:24Katika miaka ya hivi karibuni, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekuwa zikikabiliwa na mizozo kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi, mizozo ambayo imezidi kuongezeka kutokana na kuendelea vita vya Russia na Ukraine, hivi kwamba sasa vita hivyo vimekuwa miongoni mwa migogoro mikuu zaidi katika umoja huo.
-
Russia yakanusha kuweko mazungumzo ya simu baina ya Putin na Trump
Nov 12, 2024 00:22Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) amekanusha taarifa zilizodai kufanyika mazungumzo ya simu baina ya rais mteule wa Marekani Donald Trump na Rais Vladimir Putin wa Russia lakini wakati huo huo amesema kuwa, Rais Putin amekuwa akisisitiza mara kwa mara kwamba hana tatizo na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi za Magharibi kama viongozi hao wataonesha nia ya kufanya hivyo.
-
Lavrov akosoa jitihada za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya Russia
Nov 11, 2024 09:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekosoa vikali njama za nchi za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya nchi hiyo.
-
Tahadhari kuhusu matokeo ya kukiukwa haki za binadamu katika kipindi kingine cha urais wa Trump
Nov 11, 2024 06:54Shirika la Human Rights Watch limetoa onyo kali likisema kuwa muhula wa pili wa urais wa Donald Trump ni tishio kubwa kwa haki za binadamu nchini Marekani na duniani kote, na kwamba taasisi huru na jumuiya za kiraia zinapaswa kumuwajibisha rais huyo mpya kuhusiana na suala hili.
-
Kushindwa tena Wazayuni, mara hii katika mitaa ya Amsterdam
Nov 11, 2024 01:05Kufuatia dharau na matusi ya mashabiki wa Kizayuni dhidi ya bendera ya Palestina baada ya kumalizika mechi ya kandanda kati ya Ajax Amsterdam na Maccabi ya Tel Aviv, vijana wanaounga mkono Palestina wamepambana vikali na Wazayuni.
-
Mtaalamu wa UN akosoa vyombo vya habari vya magharibi kwa kuficha ghasia za Waisraeli Amsterdam
Nov 10, 2024 08:00Mtaalamu wa sheria wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa vyombo vya habari vya Magharibi kuchunguzwa kwa "kuficha" utangazaji wa habari kuhusu ghasia zilizoibuliwa siku ya Ijumaa na mashabiki wa utawala wa Israel katika mji wa Amsterdam nchini Uholanzi.
-
Zaidi ya mawaziri 40 wa Afrika wakutana nchini Russia
Nov 09, 2024 07:08Mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano wa Russia na Afrika umeanza leo katika mji wa pwani wa Sochi, kusini mwa Russia; kuashiria muundo mpya wa kawaida wa mazungumzo kufuatia mikutano ya kilele kati ya pande mbili hizo.
-
WHO yanaonya juu ya kuongezeka mashambulio ya virusi vya mtandaoni dhidi ya hospitali
Nov 09, 2024 09:39Shirika la Afya Duniani (WHO) na nchi hamsini zimeonya juu ya kuongezeka mashambulizi ya virusi vya kuombea vikombolea (ransomware) dhidi ya hospitali.
-
Uhispania yazuia meli 2 za Kimarekani zinazobeba silaha za Israel kutia nanga kwenye bandari yake
Nov 09, 2024 09:16Uhispania imekataa kuruhusu meli 2 za Marekani kutia nanga kwenye bandari yake kwa sababu zimebeba silaha kwa ajili ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina na Lebanon.