-
Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora lenye uwezo wa kufika kambi za Marekani bahari ya Pasifiki
Apr 02, 2024 22:46Korea Kaskazini imefanya jaribio la kombora la masafa ya kati (IRBM) kutoka pwani yake ya mashariki, kuonyesha dhamira yake ya kuendeleza teknolojia ya makombora yenye uwezo wa kufikia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Magharibi mwa Bahari ya Pasifiki.
-
Hatua mpya ya BRICS kufuta sarafu ya dola ya Marekani
Apr 02, 2024 22:44Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoibukia kiuchumi inajadili uwezekano wa kubuni mfumo huru wa malipo unaozingatia sarafu za kidijitali ili kupunguza utegemezi kwa mifumo ya fedha ya nchi za magharibi.
-
Naibu Katibu Mkuu wa UN: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome
Apr 02, 2024 02:50Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uratibu wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za kibinadamu Ghaza, hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.
-
Utawala wa Kizayuni washambulia jengo la ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria
Apr 01, 2024 23:23Utawala ghasibu wa Kizayuni umetekeleza shambulio la anga dhidi ya jengo la ubalozi mdogo wa Iran karibu na ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Damascus Syria.
-
Mbunge wa Marekani ataka kadhia ya Ghaza imalizwe kama zilivyofanyiwa Hiroshima na Nagasaki
Apr 01, 2024 23:18Tim Walberg, Mbunge wa jimbo la Michigan Kusini nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amelazimika kufuta kauli aliyotoa ya kutaka Ukanda wa Ghaza uliozingirwa, ambao ni makazi ya zaidi ya watu milioni mbili, ushughulikiwe kama ilivyofanyiwa miji ya Nagasaki na Hiroshima ya Japan ambayo ilishambuliwa na Marekani kwa mabomu ya nyuklia.
-
Msaada mpya wa silaha wa Marekani kwa Israel wa kufanyia mauaji makubwa zaidi ya kimbari ya Wapalestina
Apr 01, 2024 07:23Sambamba na juhudi zinazofanywa kimataifa kwa lengo la kusimamisha mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni; na mashinikizo yanayotolewa kwa utawala huo uhakikishe unaruhusu kuingizwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza, duru za habari za Marekani zimeripoti kuwa serikali ya Washington imeidhinisha kupatiwa Israel shehena mpya ya silaha za kisasa ili kuweza kuua idadi kubwa zaidi ya Wapalestina.
-
Corbyn: Kuendelea Uingereza kuipa Israel silaha kunaifanya mshirika katika mauaji ya kimbari Gaza
Apr 01, 2024 07:14Kiongozi wa zamani wa chama cha Labour nchini Uingereza amezikosoa nchi za Magharibi - hasa Marekani na Uingereza - zinazoendelea kuipatia Israel silaha za kuwaua Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na kusema kuwa nchi hizo zinakiuka sheria za kimataifa.
-
Shambulizi la Moscow... Russia yaitaka Kiev kumkabidhi mkuu wa usalama
Apr 01, 2024 07:13Russia imeitaka Ukraine kuwakabidhi raia wake kadhaa, akiwemo Mkuu wa Idara ya Usalama ya nchi hiyo, kwa madai kwamba walihusika na vitendo vya "kigaidi" katika ardhi ya Russia, suala ambalo Kiev imelitaja kuwa takwa"lisilo na thamani".
-
UNICEF yaonya kuhusu hali ya kutisha ya vita kwa watoto wa Ghaza
Apr 01, 2024 03:21Msemaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto ameonya kuhusu hali mbaya na ya kutisha waliyo nayo watoto wa ukanda wa Ghaza ambao wanateseka kwa mambo mengi ikiwemo njaa na mashambulizi ya mfululizo ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni.
-
Wataalamu na wanasiasa: Israel haidhibitiki, asiyeiadhibu ni mshirika katika uhalifu
Mar 31, 2024 23:51Wataalamu na wanasiasa wanasema Israel imefikia hatua ya unazi ambayo haiwezi kuvumiliwa na kwamba Marekani, nchi za Magharibi na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ni washirika katika jinai zinazofanywa na utawala huo zikiwemo nchi za Kiarabu ambazo hazikuchukua hatua yoyote kuiadhibu Israel baada ya uamuzi wa hivi karibuni wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa ulazima wa kusitisha mapigano mara moja huko Gaza.