-
Ufaransa, Misri na Jordan zapinga shambulio la Rafah na kuunga mkono usitishaji vita Gaza
Mar 31, 2024 22:47Mkutano wa pande tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na Ufaransa ulifanyika Jumamosi Cairo, mji mkuu wa Misri, kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika vita vya Gaza na mashauriano ya kusitisha mapigano hayo.
-
Maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na Gaza yafanyika katika nchi mbalimbali
Mar 31, 2024 07:58Wananchi huko Italia, Norway, Marekani, Japan na Morocco kwa mara nyingine tena wameandamana kulaani mauaji ya kimbari ya raia wa Palestina yanayofanywa na wanajeshi ghasibu wa utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza.
-
Wananchi wa Uturuki washiriki katika uchaguzi muhimu wa serikali za mitaa
Mar 31, 2024 07:41Vituo vya kupigia kura nchini Uturuki vilifunguliwa mapema leo asubuhi kuruhusu wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotajwa kuwa ni mtihani muhimu kwa Rais Recep Tayyip Erdogan wa nchi hiyo. Weledi wa mambo wanasema kuwa Rais wa Uturuki anakabiliwa na kibarua kigumu ili kuyarejesha maeneo muhimu ya mijini aliyoshindwa na upinzani miaka mitano iliyopita.
-
Watu masikini na wakimbizi wafukuzwa Paris kabla ya Olimpiki
Mar 31, 2024 02:58Takriban wakimbizi 500 na watu masikini wasio na makazi wamehamishwa kwa nguvu kutoka mji mkuu wa Ufaransa na kupelekwa maaeneo ya vijijini na miji midogo nchini humo huku Paris ikijiitayarisha kuandaa Olimpiki ya Majira ya joto ya 2024 mnamo Julai na Agosti.
-
Zelensky aonya: Bila msaada wa kijeshi wa Marekani, Ukraine italazimika kurudi nyuma
Mar 30, 2024 22:47Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema iwapo nchi yake haitopatiwa msaada wa kijeshi ulioahidiwa na Marekani ambao kwa sasa umezuiwa kutokana na mizozo iliyomo ndani ya Kongresi ya nchi hiyo italazimika kurudi nyuma katika vita na Russia hatua kwa hatua.
-
Siku ya Kimataifa ya Quds; mkusanyiko wa Waislamu duniani kote kutangaza mshikamano na wananchi wa Palestina
Mar 30, 2024 22:44"Siku ya Kimataifa ya Quds" mwaka huu ina umuhimu mahsusi kwa Waislamu katika nchi mbalimbali kwa kuzingatia matukio ya Gaza; ambapo Waislamu wataweza kutangaza mshikamano wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina na kuweka wazi kwa walimwengu jinai za utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake, kwa kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika miji mbalimbali duniani.
-
Ripoti: Magaidi walioua watu 143 Moscow walipokea maagizo kutoka Ukraine
Mar 30, 2024 07:35Ripoti ya wachunguzi wa Russia imethibitisha kuwepo ushahidi kwamba magaidi walioshambulia ukimbi wa Crocus jijini Moscow walipokea fedha kwa siri kutoka Ukraine, nchi muitifaki wa Marekani ambayo iko vitani na Russia.
-
Kama walivyomfanyia Ozil, mrengo wa siasa kali za kulia Ujerumani watumia kidole cha shahada cha Rudiger kuwashambulia Waislamu
Mar 30, 2024 04:08Kundi la siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani limezusha mzozo mkubwa nchini humo baada ya kumhusisha mchezaji wa soka Muislamu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Antonio Rudiger, na "makundi ya kigaidi" kwa sababu tu ameonekana kwenye picha ya Instagram akiwa amevaa kanzu nyeupe juu ya mswala, akiinua juu kidole chake cha shahada.
-
Ikulu ya White House yalalamika, wanahabari wanaiba vyombo vya ndege ya rais
Mar 30, 2024 03:51Ripoti ya vyombo vya habari vya Marekani imefichua hali iliyoenea ya wizi wa mali na vyombo vya chumba cha waandishi wa habari kwenye ndege ya Rais wa Marekani "Air Force One" wakati waandishi wa habari wanaposafiri na rais, jambo ambalo limezua taharuki mjini Washington, DC.
-
Polisi wa Malaysia wanamkamata Muisraeli aliyepanga mauaji ya kigaidi
Mar 30, 2024 03:50Polisi ya Malaysia imemezuia operesheni ya mauaji ya kigaidi yaliyokuwa yamepangwa na shirika la ujasusi la Israel (Mossad) katika ardhi ya nchi hiyo.